Pata taarifa kuu
EU-BURUNDI-SIASA-VIKWAZO

EU yatoa mwezi mmoja kwa Burundi kuwa imeanza mazungumzo

Umoja wa Ulaya (EU) umeamua rasmi Jumatatu hii, Oktoba 26, kuanzishwa kwa mashauriano juu ya mustakabali wa ushirikiano na Burundi, inayokumbwa na mgogoro mkubwa tangu Aprili mwaka huu.

Makao makuu ya Baraza la Umoja wa Ulaya, Brussels.
Makao makuu ya Baraza la Umoja wa Ulaya, Brussels. Szilas/Wikipedia/Commons
Matangazo ya kibiashara

Barua imetumwa kwa maana hiyo, kwa Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza kwa kuwaalika viongozi wa Burundi kushiriki katika mazungumzo hayo mjini Brussels ambayo yanapaswa kuanza ndani ya siku 30. Utaratibu unaweza kusababisha kusimamishwa kwa misaada ya Ulaya.

Mashauriano yataendeshwa chini ya Ibara ya 96 ya Mkataba wa Cotonou. Mashauriano haya yana lengo la kuruhusu kwa serikali kuwasilisha mpango ambao utapelekea, kwa mujibu wa Umoja wa Ulaya, kuheshimu misingi ya demokrasia na haki za binadamu, lakini pia kuleta pande zote zinazozana Burundi kwenye meza ya mazungumzo. Kudhibiti au la misaada ya Ulaya kwa serikali ya Burundi inategemea. Tangu kuanza kwa mgogoro, hakujawahi kuwa na shinikizo kama hili kwa serikali ya Bujumbura.

Chochote kinawezekana katika ajenda ya mazungumzo na kuongezeka kwa shinikizo. Kama alivyopongeza Smail Chergui, kamishna wa Amani na Usalama wa Umoja wa Afrika, "Inaleta matumani kuona jumuiya ya kimataifa inasimama kidete na kuzungumzia kwa sauti moja juu ya Burundi," Smail Chergui ameandika kwenye Twitter.

Hivi karibuni Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika na Umoja wa Ulaya vilichukua maamuzi makali kuhusiana na Burundi ili kuishinikiza serikali ya nchi hiyo kuanzisha mazungumzo na pande zingine katika mgogoro huo unaoendelea, katika matumaini ya kukomesha vurugu na hasa kuepuka machafuko mabaya ambayo yanaweza kutokea wakati wowote, msemaji wa mashauriano ya Umoja wa Ulaya, Catherine Ray , amebaini.

" Hali ya usalama nchini Burundi imedorora katika kipindi kiliyotangulia uchaguzi wa bunge na rais mwezi Juni na Julai. Harakati za mazungumzo ya kisiasa ziliongezwa, kabla ya uchaguzi, kwa lengo la kujenga makubaliano ya kisiasa juu ya mchakato wa uchaguzi lakini, katika hatua hii, inaonekana kwamba hali inaendelea kudorora ; ukiukwaji wa haki za binadamu unaendelea kushuhudiwa hapa na pale ", Catherine Ray ameiambia RFI.

" Kama mnavyojua, hivi karibuni Umoja wa Ulaya pia ulichukua hatua dhidi ya watu wanne ambao wanaonekana kuwa wanahusika katika vurugu, na kwa sababu hizi zote, imeamuliwa leo kuanzishwa mashauriano hayo ili kuleta pande tofauti kwenye meza ya mazungumzo ili kuepuka, kwa kweli, vurugu na kuziweka pamoja pande zote zinazozozana nchini Burundi kwa kujadili namna ya kupata suluhu ambayo ni ya kisiasa ", ameongeza msemaji wa mashauriano ya Umoja wa Ulaya.

" Hatua yetu inakwenda sambamba katika msaada wa juhudi za jumuiya ya kimataifa na hasa zile za Jumuiya ya Afrika Mashariki na Umoja wa Afrika. Ni muhimu sote kujaribu, kushinikiza katika mwelekeo, na hayo yote yameanza kufanyika ",Catherine Ray, msemaji wa mashauriano ya Umoja wa Ulaya amemalizia.

Aina ya vikwazo

Shinikizo zinaelekezwa katika sehemu tatu muhimu. Kwanza, vikwazo vinavyowalenga watu binafsi. Marekani na Umoja wa Ulaya tayari wamechukua vikwazo hivyo. Kwa upande wake, Umoja wa Afrika unaandaa orodha kwa ajili ya kupitishwa.

Sehemu ya pili inahusu kusimamishwa kwa ushirikiano. Baadhi ya nchi tayari zimefanya hivo kama Ubelgiji na Ujerumani, lakini pamoja na kutumwa kwa barua ya mwaliko kwa Rais Pierre Nkurunziza kwa mashauriano ndani ya siku 30, kwa mujibu wa Ibara ya 96 ya Mkataba wa Cotonou. Umoja wa Ulaya ni mfadhili mkuu wa Burundi, ambao unatoa 50% katika bajeti ya nchi hiyo. Marekani pia tayari imetangaza kwamba itapitia upya ushiriki wa Burundi katika mpango wa AGOA.

Na uamzi wa mwisho wa jumuiya ya kimataifa, iwapo machafuko yataendelea, ni kuhamishwa kwa wanajeshi na askari polisi wa Burundi katika operesheni za kulinda amani.

Hadi Jumatatu alaasiri wiki hii, Ofisi ya rais wa Burundi imesema bado haijapokea barua na inajizuia kutoa majibu kwa siku za baadaye.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.