Pata taarifa kuu
UGANDA-BURUNDI-MAZUNGUMZO-SIASA

Uganda yatangaza kuitisha mazungumzo kati ya wanasiasa wa Burundi

Wakati hali ya wasiwasi ikiendelea kuripotiwa nchini Burundi, ambapo kila kukicha kumekuwa kukiripotiwa vifo vya watu wanaopoteza maisha hasa katika mazingira tatanishi.

Wapinzani dhidi ya muhula wa tatu wa rais Pierre Nkurunziza wakiandamana Bujumbura, Juni 4 mwaka 2015.
Wapinzani dhidi ya muhula wa tatu wa rais Pierre Nkurunziza wakiandamana Bujumbura, Juni 4 mwaka 2015. REUTERS/Goran Tomasevic
Matangazo ya kibiashara

Juhudi za kuishinikiza serikali ya nchi hiyo kuitisha mazungumzo na wadau wote wa kisiasa kumaliza mzozo huo, zinaendelea.

Tayari Serikali ya Uganda imetangaza kuitisha mazungumzo kati ya wanasiasa wa Burundi, jijini Kampala, nchini Uganda, mwezi ujao wa Novemba. Mikutano ya awali kuhusu kupanga orodha ya wataoshiriki imekuwa ikifanyika tangu Jumatatu juma hili.

Hata hivyo msemaji wa serikali ya Uganda, Ofwono Opondo, hakutoa taarifa zaidi kuhusu mikutano hiyo na hata majina ya wanaopendekezwa kushiriki katika mazungumzo hayo.

Waziri wa mambo ya nje wa Burundi Alain Aimé Nyamitwe amesema kushtushwa na hatuwa hiyo kwani hivi karibuni aliwasiliana na waziri wa ulinzi wa Uganda Cruspus Kiyonga ambae ni msuluhishi wa mgogoro wa Burundi, lakini hawakuzungumzia lolote kuhusu majadiliano hayo.

Itafahamika kwamba mwishoni mwa juma lililopita Umoja wa Afrika umetangaza kuwa uko mbioni kuwachukulia vikwazo baadhi ya viongozi wa serikali ya Burundi wanaoendelea kuchochea machafuko na kukiuka haki za binadamu.

Umoja huo pia uliitaka serikali ya Burundi kuanzisha mazungumzo yatakayowashirikisha wadau wote, na wale waliokimbilia nje ya nchi, na kubaini kuwa mazungumzo hayo yanapaswa kufanyika nje ya nchi, hasa nchini katika mji mkuu wa Uganda, Kampala au mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.