Pata taarifa kuu
BURUNDI-EU-VIKWAZO-USALAMA

EU yataka kuanzisha mashauriano na Burundi

Nchini Burundi, Rais Pierre Nkurunziza anatazamia kupokea Jumatatu ijayo barua kutoka kwa mkuu wa mashauriano ya kigeni wa Umoja wa Ulaya, Federica Mogherini. Barua muhimu kwa mahusiano ya baadaye ya ushirikiano kati ya nchi ishirini na nane na Burundi. Barua ambayo shirika la habari la Ufaransa la AFP limepata kopi.

Makao makuu ya Umoja wa ulaya, Brussels.
Makao makuu ya Umoja wa ulaya, Brussels. Getty Images
Matangazo ya kibiashara

Mwanadiplomasia mmoja kutoa nchi ya Magharibi ana imani kuwa mashauriano hayo hayawezi kunusuru mahusiano ambayo tayari yamesha ingiliwa na mvutano kati ya Umoja wa Ulaya na viongozi wa Burundi. Katika rasimu ya barua hiyo ambayo itathibitishwa kutumwa Jumatatu wiki ijayo katika Baraza la Umoja wa Ulaya, mkuu wa mashauriano ya kigeni wa Umoja wa Ulaya ameomba mashauriano na viongozi wa Burundi kwa lengo la " kuchunguza kwa kina hali inayojiri nchini humo,na kamaitahitajika kuchukua hatua za kukabiliana nayo. "

Federica Mogherini amependekeza hatua hizo ziandaliwe mjini Brussels kwa " tarehe watakayokuabaliano wote kwa pamoja" . " Mashauriano hayo yatafanyika kwa mujibu wa Ibara ya 96 ya Mkataba wa Cotonou, Ibara inayotoa masharti kwa kusimamishwa kwa ushirikiano katika masuala ya kutozingatia kanuni fulani katika suala la demokrasia na haki za binadamu.

Majibu yanatarajiwa ndani ya siku 30

Baada ya kupokea barua hiyo, Rais Nkurunziza atakuwa na siku thelathini kujibu na kuthibitisha tarehe ya mkutano wa kwanza mjini Brussels. Kutakuwa na siku 120 kwa mashauriano hayo. Lengo lao: kuwawezesha Burundi kuwasilisha mpango, hasa kuhusiana na kanuni za kidemokrasia na haki za binadamu, katika mtazamo wa Umoja wa Ulaya.

Adhabu zitatekelezwa, kama hakuna majibu ndani ya muda uliyopangwa au " iwapo hakutofikiwa suluhu maridhawa " ni moja kwa moja kusimamishwa kwa ushirikiano. Adhabu ambayo ni kubwa kwa nchi ambayo inategemea nusu ya msaada wa kimataifa katika bajeti yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.