Pata taarifa kuu
TANZANIA-UCHAGUZI-SIASA

Uchaguzi Tanzania: watu wajitokeza kwa wingi Dar es Salaam

Watanzania wamepiga kura Jumapili mwishoni mwa juma hili. Uchaguzi wa rais uliofanyika katika duru moja na umewavutia wagombea wanane na ushindani mkubwa umekua kati ya mgombea wa chama tawala cha CCM, John Magufuli, na Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowasa.

Zoezi la uhesabuji wa kura limeanza shughuli katika kituo kimojacha kupigia kura Dar es Salaam, Oktoba 25, 2015.
Zoezi la uhesabuji wa kura limeanza shughuli katika kituo kimojacha kupigia kura Dar es Salaam, Oktoba 25, 2015. AFP/DANIEL HAYDUK
Matangazo ya kibiashara

Lowasa hivi karibuni alijiunga na chama cha upinzani cha CHADEMA chini ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).

Chaguzi zote zimefanyika kwa pamoja ikiwa ni pamoja na uchaguzi wa wabunge na uchaguzi wa manispaa. Takwimu za watu walioshiriki uchaguzi huo hazijatolewa lakini jijini Dar es Salaam, watu wameitikia kwa wingi, kama walivyoshuhudia waandishi wa RFI katika maeneo mbalimbali ya mji huo.

Watanzania wengi wana moya ya uzalendo kwa kukubali kusubiri hadi masaa manne katika jua kabla ya kuweza kupiga kura. Katika maeneo ya matajiri yenye wakazi wa dogo, zoezi limeendelea kwa haraka, lakini katika vitongoji mbalimbali kumeonekana misururu ya watu. Baadhi ya meneo wapiga kura wameoneka wengi na imechukua muda mrefu ili zoezi hilo lifaulu.

Katika eneo la Kimara Temboni, jijini Dar es salaam kufikia mchana leo hakuna chochote kilichokuwa kinaendelea baada ya vifaa vya kupigia kura kama makaratasi na masanduku.

Vituo kadhaa vya kupigia kura katika maeneo ya Magomeni, Manzese na Chuo Kikuu cha Dar es salaam na baadhi ya wapiga kura walikosa majina yao katika orodha ya kupigia kura.

Magufuli alipiga kura nyumbani kwao katika kijiji cha Chato katika eneo la Kanda ya Ziwa, huku Lowasa naye akipiga kura nyumbani kwao huko Monduli Kaskazini mwa nchi hiyo.

Mbali na Tanzania bara, uchaguzi huu pia unaendelea visiwani Zanzibar na ushindani mkali ni kati ya rais anayemaliza muda wake Mohamed Shein na Maalim Seif Shariff wa upinzani chama cha CUF.
Ilikua inatazamiwa kuwa Kura zingelianza kuhesabiwa baada ya kumalizika kupiga kura saa 10 jioni saa za Afrika Mashariki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.