Pata taarifa kuu
TANZANIA

Mamilioni ya Watanzania wapiga kura

Watanzania wapatao Milioni 22 nukta 7 wanapiga kura katika uchaguzi wa kihistoria kuwachagua wabunge, madiwani na rais.

Raia wa Tanzania akipiga kura
Raia wa Tanzania akipiga kura rfi kiswahili
Matangazo ya kibiashara

Zoezi la kupiga kura lilianza vema katika maeneo mengi katika nchi hiyo ya nchi hiyo ya Afrika Mashariki kuanzia saa moja asubuhi na vituo vinafungwa saa kumi jioni.

RFI Kiswahili ilitembelea vituo kadhaa vya kupigia kura katika maeneo ya Magomeni, Manzese na Chuo Kikuu cha Dar es salaam na baadhi ya wapiga kura walikosa majina yao katika orodha ya kupigia kura.

Mpira kura
Mpira kura

Katika eneo la Kimara Temboni, jijini Dar es salaam kufikia mchana leo hakuna chochote kilichokuwa kinaendelea baada ya vifaa vya kupigia kura kama makaratasi na masanduku.

Uchaguzi huu umewavutia wagombea wanane wa urais na ushindani mkali inatarajiwa kuwa kati ya mgombea wa CCM John Pombe Magufuli na Edward Lowasa wa CHADEMA chini ya umoja wa Katiba ya wananchi Ukawa.

Magufuli alipiga kura nyumbani kwao katika kijiji cha Chato katika eneo la Kanda ya Ziwa, huku Lowasa naye akipiga kura nyumbani kwao huko Monduli Kaskazini mwa nchi hiyo.

Mbali na Tanzania bara, uchaguzi huu pia unaendelea visiwani Zanzibar na ushindani mkali ni kati ya rais anayemaliza muda wake Mohamed Shein na Maalim Seif Shariff wa upinzani chama cha CUF.

Kura zitaanza kuhesabiwa baada ya kumalizika kupiga kura saa 10 jioni saa za Afrika Mashariki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.