Pata taarifa kuu
TANZANIA-UCHAGUZI-SIASA

Tume ya uchaguzi Tanzania yasema iko tayari kwa uchaguzi

Watanzania wanapoendelea kusubiri kupiga kura siku ya Jumapili, Mahakama Kuu jijini Dar es salaam inatarajiwa kutoa ufafanuzi wa ikiwa ni kisheria mpiga kura ataweza kusalia mita mia mbili baada ya kupiga kura au kwenda nyumbani baada ya kumaliza zoezi hilo.

Dar es Salaam  mji mkuu wa Tanzania,  ambayo inajiandalia uchaguzi Jumapili Oktoba 25.
Dar es Salaam mji mkuu wa Tanzania, ambayo inajiandalia uchaguzi Jumapili Oktoba 25. Getty Images/Ariadne Van Zandbergen
Matangazo ya kibiashara

Tume ya uchaguzi imewataka wapiga kura kurudi nyumbani baada ya kupiga kura lakini chama cha upinzani CHADEMA kimetaka wafausi wao kusalia mita mia mbili baada ya kupiga kura kwa kile wanachosema ni kulinda kura.

Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini humo Jaji Mstaafufu Damian Lubuva ameiabia RFI Kiswahili kuwa tume yake iko tayari kwa uchaguzi huo.

Wakati huo kampeni za uchaguzi zinaendelea nchini Tanzania wakati zikisalia siku tano ili uchaguzi mkuu ufanyike.

Hayo yakijiri mgombea urais wa chama tawala nchini Tanzania CCM John Magufuli ameshtumu vitendo vya kuwauawa watu wanaoishi na ulemavu wa ngozi nchini humo Al Bino ili kufanikiwa kisiasa au kibiashara , na kusema ni jambo ambalo halikubaliki kamwe.

Watu wanaoishi na ulemavu wa ngozi Tanzania wakabiliwa na mauaji kutokana na imani za kishirikina, Dar-es-Salaam, Mei 5, 2014.
Watu wanaoishi na ulemavu wa ngozi Tanzania wakabiliwa na mauaji kutokana na imani za kishirikina, Dar-es-Salaam, Mei 5, 2014. PHOTO/MILLIYET DAILY HANDOUT/BUNYAMIN AYGUN

Akifanya kampeni katika Wilaya ya Sengerema ambayo kumekuwa na ripoti za kuwavamia Al bino, Magufuli amesema uvamizi na mauaji hayo ni lazima yakome kwa sababu yanaiabisha Tanzania.

Kwa umoja wa yakwimu za Umoja wa Mataifa, Al Bino 76 wameuawa tangu mwaka 2000 katika taifa hilo la Tanzania kwa kile kinachoaminiwa kuwa ni kwa sababu za imani za kishirikina.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.