Majeshi ya Uganda yaondoka Sudan Kusini
Kundi la kwanza la jeshi la Uganda linatarajiwa kuwasili nyumbani leo Jumatano likitokea nchini Sudan Kusini.
Imechapishwa:
Ripoti zinasema kuwa kundi hilo limekuwa likipiga kambi katika mji wa Bor Kilomita 190 Kaskazini mwa mji wa Juba.
Hatua hii inakuja katika utekelezwaji wa mkataba wa amani kumaliza machafuko nchini Sudan Kusini, ambao ulitaka wanajeshi wa Uganda kuondoka nchini humo.
Msemaji wa jeshi hilo la UPDF, Luteni Kanali Paddy Ankunda, amesema Sudan Kusini haitakuwa na sababu ya kutotekeleza mkataba huo wa amani baada ya jeshi la Uganda kuondoka kabisa nchini mwao.
Mapigano nchini Sudan Kusini yamesababisha vifo vya maefu ya watu, huku mamia kwa maelfu ya raia wakiyahama makaazi yao.
Machafuko nchini Sudani Kusini yalilipuka kufuatia ogomvi wa madaraka kati ya Rais Salva Kiir na aliye kuwa makamu wake Riek Machar, ambao wote ni kutoka makabila mawili tofauti.