Pata taarifa kuu
UGANDA-Diplomasia

Uganda inakiri kwa mara ya kwanza kuwatuma wanajeshi wake nchini Sudan Kusini kumsaidia Salva Kiir

Serikali ya Uganda imethibitisha kwamba wanajeshi wake walitumwa hivi karibuni kushirikiana na jeshi la serikali ya Sudan Kusini katika mapigano kati ya jeshi linalomuunga mkono rais Salva Kiir na wanajeshi walioasi wanaomuunga mkono alie kua makamo wa rais Riek Machar, huku shirika la kimataifa linalotetea haki za binadamu likilani mauwaji ya kikabila, ambayo yamekua yakishuhudiwa katika taifa hilo changa.

RFI
Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo ya kusaka amani na kukomesha mapigano kati ya wajumbe wa serikali ya Juba na wale wa Riek Machar aliefutwa kazi mwezi wa julai bado yanasuasua mjini Addis-Ababa, nchini Ethiopia.

Hakuna taarifa mpya kuhusu mapigano, ambayo yanaingia kwa mwezi wa pili sasa.
Nchi ya Uganda, ambayo ni moja kati ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya mataifa ya Afrika ya Mashariki (IGAD), imekua mpatanishi fika katika mazungumzo yanayoendelea mjini Addis-Ababa.

Lakini rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni, amekubali kwa mara ya kwanza hadharani kwamba Uganda ilipata hasara kwa wanajeshi wake wanaoshirikiana na jeshi la Sudan Kusini kwa dhidi ya waasi wanaomuunga mkono Riek Machar.

“Kwa siku moja tu ya januari 13 jeshi la Sudan Kusini likishirikiana na wanajeshi wetu, tulifaulu kuteka baadhi ya maeneo yaliyokua yakishikiliwa na waasi, badhi ya waasi walipoteza maisha karibu kilomita 90 na mji wa Juba, na kwa kweli hata upande wa jeshi letu tulipata hasara baada ya kuwakosa baadhi ya wanajeshi ambao waliuawa na waasi”, amesema Yoweri Museveni jana jumatano katika kikao cha kikanda mjini Lunada, nchini Angola.

“Wakati huo waasi wengi waliuawa, na upande wetu wanajeshi kadhaa waliuawa na wengine walijeruhiwa”, ameendelea kusema Museveni.

Serikali ya Uganda ilituma kikosi cha wanajeshi nchini Sudan Kusini siku 5 baada ya mapigano hayo kuanza, desemba 15 kwa lengo la kuwaondoa raia wake waliyokua wakiishi nchini humo na kumsaidia Salva Kiir, lakini Kampala ilisalia kimya bila hata hivo kufahamisha lengo la kutumwa kwa wanajeshi wake nchini Sudan Kusini.

limefahamisha leo kundi la viongozi wa kidini na wasomi, katika tangazo waliyotoa.

“Uhasama wa kisiasa ulibadika na kua machafuko ambayo yalienea nchi nzima”, limefamisha shirika moja la kiraia liitwalo Citizens for Peace and Justice.

Mpigano hayo yamesababisha maelfu ya watu kupoteza maisha na wengine 400,000 kulazimika kuyahama makaazi yao.

Katika ripoti iliyotolewa na shirika la kimataifa linalotetea haki za binadamu Human Rihgt Watch linaonesha kua raia wasiyo kua na hatia walilengwa kutokakana na jamii wanakotoka.

Shirika hilo linabaini kwamba desemba 16, watu kutoka jamii ya Nuer kati ya 200 na 300 waliuawa mjini Juba na jeshi la serikali wakati watu hao walikua wakijaribu kukimbia mapigano hayo.

Human Right Watch imebaini pia kwamba watu kutoka jamii ya Dinka waliuawa na wwasi wanomuunga mkono Riek Machar.

D'autres informations citent des meurtres ciblés dont ceux d'enfants.

Kuna taarifa ambazo zinafahamisha kwamba watoto waliuawa katika mapigano hayo.

Jeshi halijatoa taarifa yoyote kuhusu jinsi hali ilivyo kwenye uwanja wa mapigano, lakini televisheni ya taifa ilisoma tangazo la jeshi linaloomba raia kuondoka mara moja katika mji wa Bor, ulioko kwenye kilomita 200 na mji wa Juba, ambao jeshi la serikali unajaribu kudhibiti.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.