Pata taarifa kuu
UGANDA-SUDAN KUSINI-Usalama

Uganda yakiri kua wanajeshi wake tisa wameuawa nchini Sudan Kusini

Wanajeshi tisa wa jeshi la Uganda, UPDF wameuawa huko Sudan Kusini huku kumi na wawili wakijeruhiwa, jeshi hilo lilingia nchini humo desemba mwaka jana ili kumusaidia Rais Sudan Kusini Salva Kiir anayepambana na wapiganaji wanaomuunga mkono Riek Machar aliyekuwa makamu wake wa rais.

Raisi wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni
Raisi wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni RFI
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Uganda Yoweri kaguta Museveni ameyatuhumu mataifa ya magharibi na baadhi ya makundi ya watu kwa kuchochea machafuko nchini humo wakitumia nafasi hiyo kutaka kuwagawa wananchi.

Mkutano wa nchi za IGAD uliokuwa ufanyike alhamisi ya juma hili umeahirishwa kwa muda, ambapo viongozi wa mataifa saba wanachama wa jumuiya hiyo ya ukanda wa afrika mashariki na kati walitarajiwa kukutana mjini Juba kujadili hali ya usalama nchini humo. 

Nchi ya Uganda ni kati ya mataifa machache barani Afrika ambayo yamepeleka wanajeshi wake nchini Sudan Kusini na kuwa mstari wa mbele kwenye uwanja wa vita kukabiliana na waasi.

Wakati huohuo hali mbaya ya misaada ya kibinadamu imeendelea kushuhudiwa nchini Sudan Kusini ambako wanajeshi wa Serikali wakisaidiwa na wanajeshi wa Uganda wameendelea kukabiliana na wapiganaji waasi wa aliyekuwa makamu wa taifa hilo Riek Machar.

Mashirika ya kutoa misaada nchini Sudan Kusini yameendelea kukabiliwa na changamoto ikiwemo kushindwa kuwafikia wananchi wote ambao wengi wamehama makazi yao na wengine wamenaswa kwenye uwanja wa vita.

Hapo jana shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na watoto UNICEF limesema kuwa misaada kwa ajili ya watoto imewasili mjini Juba ambapo baadae misaada hiyo itasambazwa kwenye maeneo ambayo watoto wengi wameathirika kutokana na mapigano yanayoendelea.

Hayo yakijiri shinikizo zaidi limeendelea kuwekwa kwa pande mbili zinazopigana nchini Sudan Kusini, ambapo wametakiwa kuhakikisha mwishoni mwa juma hili wanatangaza kusitisha mapigano nchini humo.

Maelfu ya raia wameuawa mpaka sasa huku mamilioni ya watu wakiyakimbia makazi yao kufuatia mapigano kati ya wanajeshi wa Serikali ya rais Salva Kiir na wale wa waasi wanaomuunga mkono aliyekuwa makamu wa rais Riek Machar.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.