Pata taarifa kuu
SUDAN-CHINA-USHIRIKIANO

Omar Al-Bashir ziarani China

Rais wa Sudan Omar al-Bashir anatarajiwa kuzuru China tarehe 3 mwezi ujao. Wizara ya Mambo ya nje imethibitisha ziara hii ya rais Bashir anayetafutwa na Mahakama ya Kimataifa ya ICC kwa tuhma za kuchochea mauaji katika jimbo la Darfur.

Fatou Bensouda (kushoto), Mwendesha mashitaka mkuu wa ICC, Hague, na Haye na Omar Al Bashir, rais wa Sudan.
Fatou Bensouda (kushoto), Mwendesha mashitaka mkuu wa ICC, Hague, na Haye na Omar Al Bashir, rais wa Sudan. AFP/Isaac Kasamani/Khaled Desouki/Montage RFI
Matangazo ya kibiashara

Bashir anatarajiwa kuondoka Khartoum leo Jumatatu na anatazamia kufanya ziara hiyo nchini China kwa muda wa siku nne.

Mara ya mwisho kwa kiongozi huyo wa Sudan kuzuru china ilikuwa ni mwaka 2011.

China sio mwanachama wa Mahakama ya ICC na hivyo haiwezi kumkata rais Bashir na kumpeleka katika Makao Makuu ya Mahakama hiyo mjini Hague.

Itafahamika kwamba miezi ya hivi karibuni rais Omar al-Bashir aliponea kukamatwa nchini Afrika Kusini alipokua akishiriki katika mkutano wa Umoja wa Afrika, baada ya shirika moja linalotetea haki za binadamu nchini humo kufikisha mashitaka mbele ya Mahakama ya Pretoria dhidi ya rais huyo. Lakini haikua rahisi Omar Al-Bashir kukamatwa kwani aliondoka nchini Afrika Kusini kwa msaada wa serikali ya nchi hiyo, licha ya Mahakama ya Pretoria kuomba vikosi vya usalama kumzuia rais Omar al-Bashir asiondoki nchini Afrika Kusini kabla ya uamzi wa Mahakama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.