Pata taarifa kuu
BURUNDI-TANZANIA-UKIMBIZI-MAANDAMANO-USALAMA

Wakimbizi 27 wa Burundi wamefariki Tanzania

Umoja wa Mataifa umesema wakimbizi 27 kutoka Burundi waliokimbilia nchini Tanzania wamepoteza maisha kwa sababu ya ugonjwa wa kipindupindu.

Makabiliano makali yameendelea kushuhudiwa jijini Bujumbura kati ya waandamanaji na polisi, Mei 20 mwaka 2015.
Makabiliano makali yameendelea kushuhudiwa jijini Bujumbura kati ya waandamanaji na polisi, Mei 20 mwaka 2015. REUTERS/Goran Tomasevic
Matangazo ya kibiashara

Maafisa wa umoja huo wamesema maelfu ya wakimbizi hao wapo hatarini na ikiwa hatua za haraka hazitachukuliwa huenda idadi ya vofo ikaongezeka katka siku zijazo.

Wanaothirika zaidi na kipindupindu ni watoto na wanawake ambao wamekimbia nchi yao kwa hofu ya ukosefu wa usalama.

Mashirika ya Kimataifa kutoka misaada ya kibinadamu kama OXFAM yamesema wakimbuzi hao wanakosa maji safi ya kunywa pamaja na ukosefu wa huduma za matibabu.

Hata hivyo wakimbizi kutoka Burundi wanaendelea kuwasili mjini Kigoma kwa meli wakitokea Kagunda.

Wanapowasili wanapelekwa katika katika kituo cha muda kabla ya kwenda katika kambi ya Nyaragusu.

Umoja wa Mataifa unasema tayari wakimbizi zaidi ya elfu hamsini wameingia nchini Tanzania kwa kuhofia usalama wao kutokana na hali ya kisiasa inayoendelea nchini Burundi.

Hayo yakijiri maandamano yaendelea katika wilaya mbalimbali za mji wa Bujumbura. Watu waandamanaji wawili waliuawa na polisi Alhamisi wiki hii. Moja aliuawa katika wilaya ya Musaga kusini mwa jiji la Bujumbura na mwengine aliuawa wilayani Ngagara kaskazini mwa jiji hilo.

Wakati huo huo Ubelgiji umetangaza kusitisha msaada wake wa moja kwa moja kwa Burundi.

Kauli hiyo imetolewa na naibu waziri mkuu na waziri wa ushirikiano wa kimataifa Alexander de Croo akihojiwa na kituo chetu cha runinga cha France 24.

Ubelgiji ni mfadhili wa kwanza wa Burundi kwa kuipa kila mwaka msaada wa zaidi ya Euro milioni 47 ambazo zitafadhiliwa kwa njia ya mashirika yasiyo ya kiserikali na mashirika ya kiraia.

Wakati hayo yakijiri, Mkurugenzi wa kituo cha binafsi cha Redio na televisheni cha Renaissance Fm anatarajiwa kuwasili leo Ijumaa kwenye mahakama ya mjini Bujumbura kwa uchunguzi kufuatia harakati za jaribio la mapinduzi, huku mkurugenzi wa Taasisi ya mawasiliano nchini humo Richard Giramaho akivitaka vyombo vya habarari kuanza kazi zao kuelekea uchaguzi.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.