Pata taarifa kuu
BURUNDI-MAANDAMANO-USALAMA-SIASA

Nkurunziza ahakikisha kuwa Burundi ina " amani na usalama "

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza amechukua uamzi wa kuahirisha kwa kipindi cha siku kumi uchaguzi wa wabunge na madiwani kama  jibu kwa upinzani na jumuiya ya kimataifa.

Mmoja wa waandamanajia akishikilia bibilia wakati wa makabiliano na polisi, Jumatano Mei 20, Bujumbura.
Mmoja wa waandamanajia akishikilia bibilia wakati wa makabiliano na polisi, Jumatano Mei 20, Bujumbura. REUTERS/Goran Tomasevic
Matangazo ya kibiashara

Katika hotuba aliyoitoa Jumatatano jioni wiki hii kwenye redio na televisheni vya taifa, rais Pierre Nkurunziza amehakikisha kuwa uchaguzi utafanyika “ kwa amani ”. Pierre Nkurunziza ametoa onyo kwa vyombo vya habari vya nchini humo na vile vya kimataifa, akivituhumu kuchochea maandamano.

Katika hotuba yake mpya kwa wananchi, hotuba ambayo ni ya tatu tangu kushindwa kwa jaribio la mapinduzi, wiki moja iliyopita, Pierre Nkurunziza ameahidi kuwa uchaguzi utafanyika kwa amani na utulivu nchini Burundi.

Rais Nkurunziza amepuuzia mbali maandamano yanayolenga kumkataza kuwania muhula wa tatu, akisema ni upuuzi mtupu. “ Burundi ina amani na usalama”, amesema Pierre Nkurunziza, akieleza kuwa maandamano ambayo ameyataja kuwa ni vurugu yanashuhudiwa tu katika kata zisiyozidi nne za mji mkuu Bujumbura kwa jumla ya vijiji na kata zaidi ya 3000 zinazounda Burundi. Hayo yanamaanisha kwa rais Nkurunziza kuwa Burundi ina amani na usalama kwa asilimia 99.9 nchi nzima.

Wakati huo huo, Pierre nkurunziza ametoa onyo kwa vyombo vya habari vya Burundi na vile vya kimataifa, ambavyo vimekua “ vikirusha matangazo kuhusu taarifa za uchochezi wa chuki na ubaguzi baina ya raia wa Burundi na kupaka matope taifa la Burundi au kuhimiza vurugu hasa katika kipindi hiki uchaguzi ".

Itafahamika kwamba vyombo vya habari vya kibinafsi nchini Burundi vilishambuliwa hivi karibuni na watu wanaoshukiwa kuwa askari polisi ambao walikua wakivalia sare ya polisi wakati wa jaribio la mapinduzi. Redio na televisheni vya taifa pamoja na redio inayomilikiwa na Kanisa Katoliki ndizo pekee zinazorusha hewani matangazo nchini Burundi.

Waaandishi wa habari watishiwa kuuawa

Onyo hilo la rais Nkurunziza linakuja wakati ambapo tayari vikosi vya usalama vimewatishi Jumatano wiki hii waandishi wa habari wa kigeni kuwa watauawa kama wanavyouawa waandamanaji iwapo hawataondoka nchini Burundi.

Vyombo vya habari vya kigeni nchini Burundi vinatuhumiwa mara kwa mara kuchochea maandamano na kurusha hewani visa vya ukiukwaji wa haki zabinadamu vinavyotekelezwa na polisi. Maripota na waandishi wa habari wa vyombo vya habari vya kimataifa wametakiwa kuripoti Alhamisi asubuhi wiki hii kwenye Baraza la Taifa linalochunguza utendaji kazi wa vyombo vya habari (CNC),. Hata hivyo ajenda ya mazungumzo haikuwekwa wazi.

Upinzani na mashirika ya kiraia vimesema kipindi cha siku kumi kiliyotolewa na rais Nkurunziza kwa kuahirisha uchaguzi hakitoshi kwa kutafutia suluhu matatizo ambayo yanaonekana kuwa kizingiti kwa uchaguzi nchini Burundi. Upinzani na vyama vya kiraia vimesema kuna suala la kuwania muhula wa tatu kwa raias Nkurunziza, ukosefu wa usalama, kuwapa silaha vijana wa chama tawala Imbonerakure, vyote hivyo ni mongoni mwa matatizo ambayo hayawezi kupelekea uchaguzi unafanyika kwa amani na usalama.

Waandamanaji wansema wataendelea kumshinikiza rais Nkuruniza kuachana na mpango wake wa kuwania urais kwa muhula wa tatu licha kuonywa kuacha maadamano hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.