Pata taarifa kuu
BURUNDI-MAANDAMANO-USALAMA-SIASA

Burundi: serikali yaahirisha uchaguzi, maandamano yaaendelea

Jumatano asubuhi wiki hii, rais wa Burundi Pierre Nkurunziza, ametia saini kwenye sheria ya kirais inayoahirisha uchaguzi wa wabunge na madiwani. Lengo ni kutuliza hasira za wapinzani kwani makabiliano yameendelea kushuhudiwa Jumatao wiki hii kati ya waandamanaji wa polisi.

Makabiliano makali yameendelea kushuhudiwa jijini Bujumbura kati ya waandamanaji na polisi, Mei 20 mwaka 2015.
Makabiliano makali yameendelea kushuhudiwa jijini Bujumbura kati ya waandamanaji na polisi, Mei 20 mwaka 2015. REUTERS/Goran Tomasevic
Matangazo ya kibiashara

Polisi imeonekana ikijaribu kuingia katika mitaa mbalimbali ya wilaya kunafanyika maandamano ya watu wanaopinga muhula wa tatu wa Pierre Nkurunziza. Polisi ilikua imelenga kuwatawanya waandamanaji ikitumia mabomu au gesi za kutoa machozi pamoja na risasi za moto. Wakti huo kulitokea makabiliano makali kati kati ya waandamanaji na askari polisi katika wilaya za Musaga, Nyakabiga, Cibitoke, Mutakura, Bwiza na Buterere.

Wilayani Musaga, waandamanaji waliwarushia polisi mawe, huku polisi ikiwatawanya waandamanaji kwa kutumia mabomu au gezi za kutoa machozi. Pande zote mbili zimekua zikipania kudhibiti barabara kuu RN7. Askari polisi walilazimika kuondoka kwenye barabara hiyo, wakati ambapo wilayani Nyakabiga, mwanajeshi mmoja ameuawa na askari polisi. Taarifa hii imethibitishwa na wanajeshi waliokutwa eneo la tukio. Ni mwanajeshi wa pili ambaye ameuawa tangu kuzuka kwa maandamano mjini Bujumbura.

Wakati huohuo vikosi vya usalama vimewatishia waandishi wa habari wa kigeni kuwa vitawaua kwa risasi za moto kama wanavyouwawa waandamanaji.

Hayo yakijiri Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza ametangaza kuwa uchaguzi umeahirishwa kwa muda wa siku 10 kutoka Maei 26 hadi Juni 5 mwaka 2015. Uamzi huu umewashangaza wengi, wakati ilikua tume huru ya uchaguzi ndio ilikua ikisubiriwa kutoa tangazo hilo. Awali Idara ya mawasiliano kwenye Ikulu ya rais ilitangaza kuwa uchaguzi huo uliahirishwa kwa kipindi cha wiki moja hadi Juni 2.

Upinzani umetupilia mbali uamzi huo wa serikali ukibaini kwamba muda huo uliyotolewa na rais Nkurunziza ni mdogo mno. Upinzani umebaini kwamba muda huo hautatosheleza kutafutia ufumbuzi suala la muhula wa tatu wa Pierre Nkurunziza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.