Pata taarifa kuu
BURUNDI-SIASA-USALAMA

Burundi: Rais Nkurunziza afanya mabadiliko katika serikali yake

Siku sita baada ya jaribio la mapinduzi kutofanikiwa, rais wa Burundi Pierre Nkurunziza amefanya mabadiliko katika serikali yake Jumatatu wiki hii. Mawaziri watatu ikiwa ni pamoja na waziri wa ulinzi jenerali Pontien Gaciyubwenge, waziri wa mambo ya nje Laurennt Kavakure pamoja na waziri wa biashara, wamefutwa kazi.

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza awafuta kazi mawaziri wa tatu, akiwemo waziri wa ulinzi jenerali Pontien Gaciyubwenge.
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza awafuta kazi mawaziri wa tatu, akiwemo waziri wa ulinzi jenerali Pontien Gaciyubwenge. AFP PHOTO / FRANCOIS GUILLOT
Matangazo ya kibiashara

Alain Nyamitwe, kaka wa Willy Nyamitwe, mshauri mkuu wa rais Nkurunziza katika masuala ya mawasiliano, ameteuliwa kuwa waziri wa mambo ya nje. Alain Nyamitwe amechukua nafasi ya Laurent Kavakure.

Emmanuel Ntahomvukiye , ambaye ni raia wa

kawaida, ameteuliwa kuwa waziri wa ulinzi, amechukua nafasi ya jenerali Pontien Gaciyubwenge. Ni kwa mara ya kwanza tangu Burundi ipate uhuru wake, raia wa kawaida kuteuliwa kuwa waziri wa ulinzi. Bii Irina Inantore ameteuliwa kuwa waziri wa biashara. Amechukua nafasi ya Marie-Rose Nizigiyimana.

Sababu za mabadiliko hayo hazijafahamishwa. Lakini inasemekana kuwa Laurent Kavakure amefutwa kazi baada ya kushindwa kushawishi jumuiya ya kimataifa kuhusu muhula wa tatu wa rais Pierre Nkurunziza

Inasadikiwa pia kuwa huenda jenerali Pontien

Gaciyubwenge amefutwa kazi kutokana na kushindwa kumkamata jenerali Godefroid Niyombare, ambaye alitangaza hivi karibuni kuuwangusha utawala wa Pierre Nkurunziza bila mafaanikio.

Mkuu wa majeshi jenerali Prime Niyongabo amepewa majukumu makubwa ya kusimamia na kuliongoza jeshi.

Hayo yakijiri, maandamano yameendelea katika wilaya mbalimbali za jiji la Bujumbura. Na kumeonekana wanajeshi wakiunga mkono waandamanaji, huku wengine wakiwaonya waandamanaji kusitisha maandamano hayo.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.