Pata taarifa kuu
NIGERIA-INEC-BOKO HARAM-Usalama

Uchaguzi wa urais katika hali ya kutatanisha Nigeria

Tume ya uchaguzi nchini Nigeria, INEC, imesema uchaguzi mkuu utafanyika siku ya Jumamosi Februari 14 mwaka 2015 kama ilivyopangwa.

Magari ya jeshi la Chad katika mji wa Fotokol kwenye mpaka na Cameroon Jumapili Februari 1, siku tatu kabla ya mashambulizi.
Magari ya jeshi la Chad katika mji wa Fotokol kwenye mpaka na Cameroon Jumapili Februari 1, siku tatu kabla ya mashambulizi. AFP PHOTO / STEPHANE YAS
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii imefikiwa baada ya rais Goodluck Jonathan kufanya mazungumzo na maafisa wakuu wa tume hiyo, ambapo ameomba kuahirishwa kwa uchaguzi huo kufwatia hofu ya kufanyika kwa mashambulizi ya Boko Haram.

Hayo yanajiri wakati wapiganaji wa kundi la kigaidi la Boko Haram wameripotiwa kuwaua zaidi ya watu mia moja katika shambulizi lililofanyika dhidi ya mji wa Fotokol nchini Cameroon Usiku wa Jumatano februari 4 kuamkia Alhamisi Februari 5.

Alhamisi wiki hii, magavana nchini Nigeria walikutana na makamishena wa tume ya uchaguzi nchini humo na kuwahakikishia kuwa uchaguzi huo utafanyika siku ya Jumamosi kama ilivypangwa.

Uchaguzi huo utafanyika pia kwenye maeneo yanayoshuhudia mashambulizi yanayotekelezwa na Boko Haram, hakutakuwa na kupanga foleni na vituo vitalindwa na watu watahamasishwa kujitokeza wakisindikizwa na vikosi vya usalama, Tume ya uchaguzi nchini Nigeria imetangaza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.