Pata taarifa kuu
SENEGAL-UPINZANI-MAANDAMANO-USALAMA

Senegal: hisia zatolea kuhusu marufuku ya kuandamana

Nchini Senegal, utawala umeendelea kushikilia msimamo wake. Maandamano ya vyama vikuu vya upinzani hayakuruhusiwa juma lililopita kwa sababu hayakuzingatia sheria, serikali imethibitisha.

Gari dogo ya rais wa zamani wa Senegal, Abdoulaye Wade ilikaidi agizo la polisi na kuvunja vizuizi viliyokua viliwekwa na polisi na kuingia katika eneo ambapo ilikua imepangwa kufanyika maandamano mjini Dakar, Jumamosi 31 janvier.
Gari dogo ya rais wa zamani wa Senegal, Abdoulaye Wade ilikaidi agizo la polisi na kuvunja vizuizi viliyokua viliwekwa na polisi na kuingia katika eneo ambapo ilikua imepangwa kufanyika maandamano mjini Dakar, Jumamosi 31 janvier. AFP PHOTO / SEYLLOU
Matangazo ya kibiashara

Mwishoni mwa wiki hii, baadhi ya wanaharakati walipuuzia uamzi uliyochukuliwa na mkuu wa jiji la Dakar la kukataza maandamano, na kusababisha kukamatwa kwa baadhi ya watu na kuzuka pia kwa makabiliano kati ya raia na polisi.

Jumamosi, Wade alionekana hadharani katika eneo moja mjini Dakar. Njia mojawepo, amesema Wade, ya kupinga dhidi ya hatua ya serikali ya kukataza maandamano.

Maandamano ya Jumatano ni tishio kwa usalama wa taifa. Na maombi ya kufanyika kwa maandamano Ijumaa na Jumamosi hayakufuata mkondo wa sheria. Haya ni maelezo yaliyotolewa na mkuu wa jiji la Dakar kwa kupiga marufuku mikusanyiko au maandamano ya vyama vikuu vya upinzani.

Katika matukio kadhaa, mashirika ya haki za binadamu yamekua yakishutumu uamzi huo wa kupiga marufuku mikusanyiko na maandamano yanayoandaliwa na mashirika ya kiraia au vyama vikuu vya upinzani.

" Kwa zaidi ya miaka miwili, viongozi wamekua wakifutilia mbali maombi ya PSD na maandamano ya raia", ameelezea masikitiko yake, Aboubacry Modji, katibu mkuu wa shirikisho la haki zabinadamu barani Afrika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.