Pata taarifa kuu
NIGERIA-BOKO HARAM-Usalama

Nigeria: jaribio jipya la Boko Haram Maiduguri

Wanamgambo wa Boko Haram wameanzisha Jumapili Februari 1, asubuhi, mashambulizi mapya katika mji wa Maiduguri, mji mkuu wa jimbo la Borno. 

Mtaa uliyobatizwa jina la Kashim Ibrahim, katika mji wa Maiduguri, mwaka 2013.
Mtaa uliyobatizwa jina la Kashim Ibrahim, katika mji wa Maiduguri, mwaka 2013. AFP PHOTO / STRINGER
Matangazo ya kibiashara

Jumapili iliyopita, wanajihadi walijaribu kuingia katika mji huo wenye wakazi milioni 2, ambao wanauchukulia kama ngome yao ya asili.

Mashambulizi hayo yamedumu masaa karibu matatu, lakini wanajihadi walitrejeshwa nyuma na jeshi pamoja na na vikosi vya kiraia vya ulinzi. Haijafahamika hasara iliyotokea katika mashambulizi hayo.

Kama ilivyokua Jumapili iliyopita, wakazi wa Maiduguri waliamshwa mapema asubuhi kwa milio ya bunduki aina ya Kalashnikovs.

Wanamgambo wa Boko Haram kutoka mashariki walijaribu kuingia katika mji wa Maiduguri.

Lakini jeshi na vikosi vya kiraia vya ulinzi walikabiliana na wanamgambo hao na baadaye walifaulu kuwarejesha nyuma, baada ya masaa matatu ya mapigano.

Huu hapa ni ushahidi uliyotolewa na Bello Duku, wa Idhaa ya Kihausa ya RFI: "Wapiganaji wa Boko Haram hawakufikia nyumba za wakazi wa mji wa Maiduguri. walikua wakifyatua risasi wakiwa kwenye barabara ya Dikwa. Wapiganaji hao walikabiliana na jeshi na vikosi vya kiraia vya ulinzi. Kwa sasa, hatuwezi hasara iliyosababishwa na mapigano hayo, kwa sababu jeshi limeuzingira mji wa Maiduguri. Hakuna mtu anaye ingia au kutoka, isipokuwa askari peke yao. Washambuliaji walielekea mashariki, ambapo wana ngome. Nadhani wameenda katika kambi yao ya Gambarou.”

Maiduguri ni suala la kimkakati. Kwa hakika ni katika mji mkuu wa jimbo la Borno ambapo lilianzishwa kundi la Boko Haram katika miaka ya 2000. Wanajihadi wanuchukulia mji huo kama ngome yao kuu. Lakini viongozi wamechukua uamzi wa kuagia majeshi ili kuulinda mji huu wenye wakazi karibu milioni moja na nusu, ikiwa ni pamoja na wakimbizi 500,000 waliyotimuliwa kutoka vijiji vya kaskazini na Boko Haram.

Hakuna maafa au majeruhi upande wa raia. hata hivyo inasemekana kuwa askari mmoja ameuawa na wengine sita wamjeruhiwa, kulingana na ushuhuda wa Profesa Khalifa Dikwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.