Pata taarifa kuu
Mauritania

Mohamed Ould Abdel Aziz achaguliwa tena rais wa Mauritania

Mohamed Ould Abdel Aziz amechaguliwa tena kuwa rais wa Mauritania baada ya kupata asilimia 81 nukta 89 ya kura za urais.

Rais wa Mauritania Mohamed Ould Abdel Aziz
Rais wa Mauritania Mohamed Ould Abdel Aziz REUTERS/Joe Penney
Matangazo ya kibiashara

Abdel Aziz amekuwa kiongozi nchi hiyo tangu mwaka 2008 baada ya kuipindua serikali, na wakati wa kampeni za urais amekuwa akinadi sera yake ya kupigana na kundi la kigaidi la Al-Qaeda nchini humo na katika eneo la Sahel.

Muungano wa upinzani nchini humo ulisusia uchaguzi huo umesema uchaguzi huo haukuwa huru na haki kama wanavyodai wafuasi wa Abdel Aziz.

Tume ya Uchaguzi inatarajiwa kumtangaza rasmi Abdel Aziz kama rais mteule baada ya mshindani wake Biram Ould Dah Ould Abeid, kupata asilimia 8 nukta 67 katika Uchaguzi huo.

Wagombea wengine, Ibrahima Moctar Sarr ameibuka katika nafasi ya tatu kwa asilimia 4 nukta 44 huku mgombea wa pekee wa kike Lalla Mariem Mint Moulaye Idriss akipata asilimia 0 nukta 49.

Tangu mwaka 2009 muungano wa upinzani ambao una vyama 11 haujawahi kukubali ushindi wa rais Abdel Aziz na wamekuwa wakishtumu kuwa Dikteta.

Waangalizi kutoka Umoja wa Afrika wanasema wameridhishwa na namna Uchaguzi huo ulivyofanyika na Uchaguzi huo ulikuwa huru na haki.

Kiongozi wa waangalizi hao Beji Caid Essebsi, ambaye pia ni Waziri Mkuu wa zamani wa Tunisia amesema “Tumeridhishwa na namna Uchaguzi ulivyofanyika kwa njia ya amani, nawashukuru raia wa Mauritania kwa kujitokeza kwa wingi,”.

Baada ya ushindi huo rais Mohamed Ould Abdel Aziz anatarajiwa kuendelea kupambana na makundi ya kigaidi nchini mwake na kuwasaidia wananchi wake kuinuka kiuchumi kutokana na raia wengi kuendelea kuwa maskini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.