Pata taarifa kuu
MAURITANIA

Matokeo ya uchaguzi yasubiriwa nchini Mauritania baada ya upigaji kura kutamatika kwa amani na utulivu

Wananchi wa Muaritani wanasubiri matokeo ya kura za kuwachagua wabunge na viongozi wa serikali za mitaa, chama cha kiislamu ndicho kinachotazamiwa kuongoza katika uchaguzi huo. Takribani wananchi milioni 3.4 wamepiga kura jana jumamosi, jumla ya wagombea 1500 kutoka vyama vya siasa 74 wamechuana kuwania viti 147 katika bunge na viti 218 vya uwakilishi wa serikali za mitaa.

EPA
Matangazo ya kibiashara

Licha ya wapinzani kupinga zoezi hizo, limetamatika kwa amani bila kuripotiwa kwa ghasia zozote mpaka hivi sasa.

Matokeo ya awali yanatarajiwa kuanza kutolewa kuanzia leo jumapili.

Rais wa nchi hiyo Mohamed Ould Abdel Aziz amesema uchaguzi huo ni ushindi katika kutafuta demokrasia ya kweli ndani ya Taifa hilo.

Rais Abdel Azizi aliingia madarakani baada ya mapinduzi ya mwaka 2008 na mwaka mmoja baadaye alishinda katika uchaguzi wa kidemokrasia, hata hivyo Taifa hilo limekuwa na hostoria ya utawala wa kijeshi toka kuanza kwa mfumo wa uchaguzi wa vyama vingi mwaka 1992.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.