Pata taarifa kuu
MAURITANIA

Upinzani nchini Mauritania walitaka jeshi kutoingilia siasa

Viongozi wa upinzani nchini Mauritania wametoa wito kwa jeshi nchini humo kukaa mbali na siasa na kutaka taarifa zaidi kuhusu afya ya raisi wa nchi hiyo.

Raisi wa Mauritania Ould Abdel Aziz,ambaye alijeruhiwa kwa risasi mnao mwezi October
Raisi wa Mauritania Ould Abdel Aziz,ambaye alijeruhiwa kwa risasi mnao mwezi October REUTERS/Darrin Zammit Lupi/Files
Matangazo ya kibiashara

Raisi Mohamed Ould Abdel Aziz, mshirika muhimu wa mataifa ya magharibi katika vita dhidi ya kundi la kigaidi la al Qaeda barani Africa,alisafirishwa kuelekea nchini ufaransa octoba 14 kwa matibabu baada ya jeraha la risasi ambalo serikali iliarifu kuwa ilifyatuliwa bila kukusudia kumlenga raisi huyo.

Hata hivyo kiongozi huyo aliruhusiwa kutoka hospitali kwa zaidi ya juma sasa lakini bado hajajitokeza hadharani nchini mauritania jambo linalozua maswali juu ya hali yake kiafya na nani anaiongoza nchi hiyo wakati huu raisi huyo akiwa nje ya ofisi.

Wafuasi kadhaa wa upinzani walijumuika jijini Noukchott alhamisi kudai uwazi kutoka kwa mamlaka kuhusu hali ya kiongozi huyo na mazingira ya kupigwa risasi.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.