Pata taarifa kuu
Libya

Mshukiwa wa mashambulizi ya ubalozi wa Marekani Benghazi, akamatwa.

Rais wa Marekani Barrack Obama anasema mshukiwa Mkuu wa mashambulizi yaliyotokea katika Ubalozi wa taifa hilo mjini Bengazi nchini Libya na kusababisha Balozi wa Marekani nchini humo mwaka 2012 amekamatwa

Mshukiwa wa Mashambulizi ya ubalozi wa Marekani Mjini Benghazi, Nchini Lybia Ahmed Abu Khattala, 17 June 2014
Mshukiwa wa Mashambulizi ya ubalozi wa Marekani Mjini Benghazi, Nchini Lybia Ahmed Abu Khattala, 17 June 2014 AFP
Matangazo ya kibiashara

Obama amesema, mshukiwa huyo Ahmed Abu Khattala alitiwa mbaroni na kikosi maalum cha Marekani na tayari ameanza kusafirishwa kwenda Marekani kujibu tuhuma zinazomkabili, amethibitisha waziri wa mambo ya nje wa Marekani john Kerry.

Msemaji wa shirika la ujasusi nchini Marekani John Kirby amemtaja Ahmed Abu Khattala kuwa gaidi nambari moja kaongeza kuwa Khattala ni miongoni mwa walioratibu mashambulizi kadhaa dhidi ya majengo yanayomilikiwa na Marekani huko Lybia.

Wakati wa mashambulizi hayo Balozi wa Marekani Chris Stevens na watu wengine watatu walipoteza maisha.

Myezi kadhaa iliyopita viongozi wa chama cha Republican walisema kuwa serikali ya Obama iliudanganya umma kuhusu tukio hilo kupitia kulihusisha na kanda moja ya video kuhusu maandamano dhidi ya raia wasio waislamu iliowekwa katika mtandao.

Baadaye ilibainika kuwa ilikuwa imepangwa na makundi ya wanamgambo.
Viongozi wa chama cha Democrates waliwashtumu wapinzani wao kwa kulifanya swala hilo la kisiasa ili kuvutia kura na ufadhili.

Marekani imesema itaendelea kupambana na ugaidi na kuwalinda raia wake ndani ya nje ya taifa hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.