Pata taarifa kuu
LIBYA

Naibu Mkuu wa Upelelezi nchini Libya, Nuh Mustafa atekwa nyara mjini Tripoli

Naibu Mkuu wa upelelezi nchini Libya, Nuh Mustafa ametekwa nyara na watu waliojihami kwa silaha mjini Tripoli, wakati mji mkuu huo ukishuhudia mgomo wa siku tatu baada ya machafuko ya maafa, yaliyosababisha hofu ya vita vya wenyewe kwa wenyewe. Maofisa Usalama wanasema Nuh alitekwa wakati akitoka katika uwanja wa ndege mjini Tripoli muda mfupi baada ya kurejea akitokea safarini.

Reuters
Matangazo ya kibiashara

Kamanda wa zamani wa waasi Ala Abu Hafess amekiambia kituo cha televisheni cha Al-Naba kuwa alikuwa katika gari moja na Mwendesha Mashtaka huyo wakati alipovamiwa.

Hofu ya usalama imeendelea kutanda nchini humo, mwezi oktoba Waziri Mkuu Ali Zeidan naye alitekwa na siku chache baadaye Kiongozi wa Ulinzi alikiri kuhusika na utekaji huo.

Baadhi ya raia wamekuwa wakiishutumu serikali kwa kushindwa kudhibiti makundi ya wanamgambo ambao walisaidia kumpindua marehemu Kanali Muammer Ghaddafi.

Mwishoni mwa juma waandamanaji waliendelea kutanda katika mji mkuu wa nchi hiyo wakishinikiza kutokomezwa kwa wanamgambo na kuimarishwa kwa jeshi, maandamano ambayo baadaye yaligeuka kuwa vurugu zinazoelezwa kuwa mbaya zaidi katika mji huo tangu mapigano ya mwaka 2011 na yale yaliyozuka siku ya ijumaa.

Kwa mujibu wa wizara ya afya, takribani watu 43 wameuawa na zaidi ya 450 kujeruhiwa katika vurugu hizo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.