Pata taarifa kuu
LIBYA

Takribani watu 10 wauawa na wengine 15 wajeruhiwa mjini Tripoli nchini Libya baada ya kulipuka kwa ghala la silaha

Watu takribani kumi wameuawa na wengine kumi na watano wamejeruhiwa vibaya mjini Tripoli nchini Libya kutokana na mlipuko wa ghala la silaha, lililovamiwa na watu waliokuwa wamejihami kwa silaha jana Alhamisi majira ya alasiri. 

Wanajeshi wa Libya wakiwa wamesambazwa kwenye eneo la tukio mjini Tripoli
Wanajeshi wa Libya wakiwa wamesambazwa kwenye eneo la tukio mjini Tripoli yourmiddleeast.com
Matangazo ya kibiashara

Gavana wa mkoa wa Brak al-Chati, Mohamed al-Dhahbi amethibitisha kuwa kikosi cha wanajeshi zaidi ya mia mbili pamoja na polisi walipelekwa katika eneo la tukio ili kulinda usalama wa ghala hiyo.

Aidha mapigano katika mji wa Mashariki mwa Benghazi yamesababisha vifo vya askari wanne mapigano amabyo yamejiri katika siku ya mwisho ya mgomo wa siku tatu dhidi ya wanajeshi wa upinzani, yaliyochochewa na mashambuliano ya risasi kati ya wanajihadi na jeshi la nchi hiyo ambayo yalisababisha vifo vya watu saba na kujeruhi 50.

Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanahisi kuwa usalama wa taifa la Libya unaendelea kuzorota tangu pale raisi Moamar El Gadaffi alipouawa, huku serikali iliyoko madarakani ikijaribu kuurejesha usalama bila ya mafanikio,

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.