Pata taarifa kuu
GUINEA BISSAU-UCHAGUZI

Guinea Bissau wanapiga kura hii leo kuamua viongozi wapya wa taifa hilo

Wapiga kura nchini Guinea Bissau wanaanza zoezi la kupiga kura hii leo kuamua atakayekuwa raisi wa taifa hilo na wabunge ili kulirejesha taifa hilo katika hali imara ya usalama baada ya kutokea kwa mapinduzi ya kijeshi.

Kituo cha kupigia kura nchini Bissau, wakati wa ufunguzi wa uchaguzi polisi na jeshi walitangulia kupiga kura
Kituo cha kupigia kura nchini Bissau, wakati wa ufunguzi wa uchaguzi polisi na jeshi walitangulia kupiga kura AFP PHOTO / SEYLLOU
Matangazo ya kibiashara

Uchaguzi huo unakuja baada ya takribani miongo minne ya ghasia zilizochangiwa na mfululizo wa maasi tangu Guinea Bissau kupata uhuru wake kutoka kwa taifa la Ureno ambapo wachambuzi nchini humo wametoa wito kwa serikali mpya itakayochaguliwa kufanya mabadiliko katika jeshi nchini humo ili kuepuka athari za mapinduzi.

Taifa hilo maskini la Afrika magharibi limekwama kwa miaka miwili chini ya utawala wa serikali ya mpito ulioungwa mkono na jeshi huku likigubikwa na hali tete kiuchumi na biashara ya madawa ya kulevya ikichochea rushwa nchini humo.

Mchambuzi wa masuala ya mizozo ya kimataifa nchini humo Vincent Foucher amebainisha kuwa serikali mpya itapaswa kuwahoji maafisa waandamizi kwa uangalifu na kufanya mageuzi katika sekta ya usalama ambayo ilisababisha kufikiwa hatua ya mapinduzi ya kijeshi.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.