Pata taarifa kuu
GUINEA-BISSAU-AU

Umoja wa Afrika AU waisimamisha uanachama nchi ya Guinea-Bissau

Kufuatia mapinduzi ya kijeshi yaliyofanyika nchini Guinea-Bissau juma lililopita, Umoja wa Afrika AU umetangaza rasmi kuisimamisha unachama wa Umoja huo nchi hiyo na kwamba inafikiria kuiwekea vikwazo. 

Wanajeshi wa Guinea-Bissau
Wanajeshi wa Guinea-Bissau Reuters
Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa tume ya usalama na amani ya AU, Ramtanae Lamamra amethibitisha tume yake kuisimamisha uanachama nchi ya Guinea-Bissau na kwamba inatarajia kuiwekea vikwazo nchi hiyo.

Umoja huo pia umeipiga marufuku nchi hiyo kujihusisha na shughuli zozote zinazosimamia na Umoja wa Afrika, hatua inayokuja wakati viongozi wa ECOWAS wako nchini humo kwajuhudi za kuwashawishi viongozi wa kijeshi kuachia madaraka kwa utawala wa kiraia.

Utawala wa Kijeshi nchini Guinea-Bissau umetangaza kufunga mipaka yake pamoja na kufunga njia za usafiri za anga na baharini wakati huu ambapo katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa UN Ban Ki Moon akilaani kuundwa kwa serikali ya mpito akisema inakuza mgogoro huo.

Katibu Mkuu wa UN Ban amesema kile ambacho kinafanyika nchini Guinea-Bissau kinastaili kuendelea kulaaniwa na kusihi utawala wa kiraia unastahili kurejeshwa ili kuepusha nchi hiyo kuwa makaburi ya watu wasio na hatia.

Katika hatua nyingine wagombea watano wa urais nchini Guinea-Bissau wameendelea kulaani mapinduzi hayo ambayo yametekelezwa na Jeshi kwa madai serikali ilikuwa na mpango wa kupunguza ukubwa wa jeshi na hivyo wanajeshi wengine wangekosa kazi.

Wagombea hao wanaendelea kukosoa mapinduzi hayo wakati ambapo ujumbe maalumu toka ECOWAS ukiwa nchini humo na jana usiku walikuwa na mazungumzo na viongozi wa utawala wa kijeshi waliofanya mapinduzi.

ECOWAS imesema haitambui mapinduzi hayo na kwamba ujumbe huo umeenda nchini humo kwa lengo moja tu, la kuwashawishi wanajeshi waliotekeleza mapinduzi kuondoka madarakani na kurejesha utawala wa kiraia.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.