Pata taarifa kuu
GUINEA BISSAU

Utawala wa kijeshi nchini Guinea Bissau wakubaliana kuunda serikali ya mpito ya miezi 12.

Askari ambao waliotwaa madaraka mwezi huu katika taifa dogo Afrika Magharibi la Guinea-Bissau wamesema kuwa wamekubaliana kuwa na serikali ya mpito kwa kipindi cha miezi 12 baada ya kufanya majadiliano na Jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi ECOWAS.

Wanajeshi wa Guinea-Bissau
Wanajeshi wa Guinea-Bissau Reuters
Matangazo ya kibiashara

Utawala huo wa kijeshi ambao hapo awali ulipendekeza kuwa na serikali ya mpito kwa miaka miwili pia wamekubali kuwaachia huru viongozi waliokuwa wamewekwa kizuizini,msemaji wa uongozi huo Daba Na Walna amebainisha.

Rais wa zamani wa serikali ya mpito Raimundo Pereira na waziri mkuu wa zamani Carlos Gomes Jr, waliokuwa wamewekwa kizuizini tangu mapinduzi ya Aprili 12, waliwasili mjini Abidjan jana Ijumaa.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.