rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Tanzania Burundi

Imechapishwa • Imehaririwa

Wakimbizi wa Burundi Tanzania walalamikia Umoja wa Mataifa

media
Wakimbizi wa Burundi waliopigwa picha Aprili 10, 2015 Rwanda. © AFP PHOTO / STEPHANIE AGLIETTI

Wakimbizi wa Burundi nchini Tanzania wameomba Umoja wa Mataifa kuingila kati kuhusu suala la kuwarejesha mwakwao bila hiari yao. Ombi hilo linakuja baada ya serikali ya Tanzania kuagiza wakimbizi kutoka nchini Burundi kurudishwa makwao, na kusema kuwa hali ya kiusalama katika taifa hilo sasa imeimarika.


Kwa upande wa mashirika ya kimataifa yanayotetea haki za binadamu yameshtumu serikali ya Tanzania kwa hatua hiyo na kubaini kwamba hatua ya serikali ya Tanzania ni kinyume na mikataba ya umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu.

Mashirika hayo yamesema yana wasiwasi kwamba wakimbizi hao wanaweza kuuawa iwapo watarejeshwa nchini Burundi.

Hata hivyo baadhi ya mashirika ya haki za binadamu yamesema yataifungulia mashitaka serikali ya Tanzania kwa kukiuka mikataba ya umoja wa mataifa kuhusu wakimbizi na kubaini kwamba itaulizwa wakimbizi hao iwapo baadhi yao watapatikana wameuawa watakaporejea nchini Burundi.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Tanzania Kangi Lugola ametangaza kuwa wakimbizi 2,000 watarudishwa Burundi kufikia Octoba mosi mwaka huu.

Tanzania ndio nchi inayohifadhi wakimbizi wengi zaidi kutoka Burundi kuliko nchi nyingine yoyote ile katika ukanda wa Afrika Mashariki.