Pata taarifa kuu
ECUADOR-TETEMEKO

Tetemeko kubwa Ecuador: watu 233 wapoteza maisha

Timu za waokozi zimekua zikijaribu Jumapili hii ili kusaidia manusura waliofunikwa na vifusi nchini Ecuador, siku moja baada ya tetemeko kubwa lenye kipimo cha 7.8 richter kiliowaua angalau watu 233.

Katika mji wa Manta, kumeshuhudiwa uharibifu mkubwa, baada ya tetemeko la ardhi lenye kipimo cha 7.8 Richter lililopiga katika mkoa wa Manabi, Ecuador, Aprili 16, 2016.
Katika mji wa Manta, kumeshuhudiwa uharibifu mkubwa, baada ya tetemeko la ardhi lenye kipimo cha 7.8 Richter lililopiga katika mkoa wa Manabi, Ecuador, Aprili 16, 2016. REUTERS/Patricio Ramos
Matangazo ya kibiashara

Katika mji wa Portoviejo (magharibi mwa Ecuador), moja ya miji ya iliothirika, nyumba kuharibiwa, soko kubaki patupu, taa zikidondoka na uchafu ukitawanyika kando ya barabara vyote hivyo vinaonyesha ukubwa wa tetemeko hilo ambalo halijawahi kutokea tangu 1979.

"Hali ilikua ya kutisha, ni mara ya kwanza ninahisi tetemeko kama hili, ni nahisi kwamba lilidumu dakika moja na nusu," Bibi Macontos, mkazi mwenye umri wa miaka 57 ameliambia shirika la habari la Ufaransa la AFP.

"Nilidhani kuwa nyumba yangu itaanguka," amesema Macontos, huku akibaini kwamba bado yuko katika hali ya mshtuko.

"Tulikwenda nje kwa haraka na kuingia mitaa na tuliona kwamba soko lililokua limefunikwa kwa bati limeporomoka," ameliambia shirika la habari la Ufaransa la AFP Nelly, mwenye umri wa miaka 73, mkazi wa Abdon Calderon, mji ulio karibu na mji wa Portoviejo, ambaye hakutaka kutaja jina lake la familia.

Katika machozi, aliiambia kwamba "kulikuwa na mtu kukwama (katika kifusi, ed) kilio kuomba msaada, lakini baada ya yeye kusimamishwa mayowe."

"Nyumba ziliporomoka, taa za mitaani zikadondokaa, watu walikata tamaa kabisa, kuna watu waliofunikewa chini ya vifusi," ameeleza Miriam Santana, mwenye umri wa miaka 40, mfanyakazi wa ndani katika mji wa Manta (magharibi mwa Ecuador).

Siku ya Jumapili, Rais Rafael Correa ametangaza ripoti mya ya muda ya watu 233 ambao wamepoteza maisha kufutia tetemeko hilo, wakati ambapo ripoti za awali za serikali ilibaini kwamba watu 77walipoteza maisha na karibu 600 wamejeruhiwa. Hali ya hatari imetangazwa.

Zaidi ya askari polisi 14,000, wataalamu wa afya 241 wametumwa katika eneo la tukio, amesema Makamu wa Rais Jorge Glas, kwa sababu "tunajua kuwa kuna watu waliofukiwa chini ya vifusi ambao wanapaswa kuokolewa". Colombia na Mexico wametuma wataalamu kusaidia nchini Ecuador.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.