Pata taarifa kuu
MAREKANI-KOREA KASKAZINI-USHIRIKIANO

Wamarekani watatu waachiliwa huru na Korea Kaskazini

Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza Jumatano wiki hii kwamba Wamarekani watatu waliokua wakishikiliwa na Korea Kaskazini, hatimaye wameachiliwa huru.

Rais wa Marekani Donald Trump huko Washington, Mei 9, 2018.
Rais wa Marekani Donald Trump huko Washington, Mei 9, 2018. AFP
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Marekani amesema kuwa Wamarekani hao wako njiani kuelekea Marekani.

"Ninafuraha kuwatangaza kwamba Wazir wa mambo ya Nje Mike Pompeo yuko njiani anarudi kutoka Korea Kaskazini na mabwana watatu ambao kila mtu ana hamu ya kukutana nao," Trump ameanika kwenye ukurasa wake wa Twitter huku akibaini kwamba anatarajia kuwapokea watakapowasili katika kambi ya Andrews karibu na Washington siku ya Alhamisi saa nane ya usiku saa za Marekani (sawa na saa 12 asubuhi saa za kimataifa.

"Wanaonekana kuwa na afya njema," Donald Trump ameongeza, akimaanisha watu hao watatu.

Rais wa Marekani ameongeza kwamba waziri wa mambo ya nje wa Marekani alikuwa na "mazungumzo mazuri" na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un. Amebaini kwamba tarehe na nafasi ya mkutano wake na kiongozi huyo wa Korea Kaskazini tayari imepangwa.

Kim Hak-Song alikuwa akifanya kazi kwa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Pyongyang (USTP) alipokamatwa mnamo mwezi Mei 2017. Alikamatwa kwenye Kituo cha Reli cha Pyongyang wakati akipanda treni kurudi nyumbani kwake, katika mji wa Dandong nchini China, kwa kushutumiwa "vitendo vya uadui" dhidi ya serikali.

Kim Sang-Duk, ambaye pia anajulikana kama Tony Kim, alikamatwa mnamo mwezi Aprili 2017 katika uwanja wa ndege wa Pyongyang wakati akijaribu kuondoka nchini baada ya kufundisha huko kwa wiki kadhaa. Pia alikua akifanya kazi kwa USTP.

Kim Dong-Chul, mfanyabiashara mwenye umri wa miaka 60 na mchungaji, alihukumiwa mnamo mwezi Aprili 2016 hadi miaka kumi ya kufanya kazi za nguvu baada ya kukamatwa kwa kosa la uasi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.