rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa
  • Mafuriko yameua watu kumi na nane Iran (idara ya hali ya Dharura)

Marekani

Imechapishwa • Imehaririwa

Wafungwa saba wauawa katika makabiliano jela Marekani

media
Mapigano yasababisha vifo vya watu saba katika jimbo la South Carolina, Marekani, Januari 17, 2012. REUTERS/Chris Keane/files

Wafungwa saba wameuawa na wengine 17 wamejeruhiwa katika mfululizo wa makabiliano katika jela la South Carolina, nchini Marekani, mamlaka imesema Jumatatu wiki hii.


Hali ya utulivu imerejea baada ya saa saba ya makabiliano katika jela la Bishopville, zaidi ya kilomita 60 kaskazini mashariki mwa mji mkuu wa jimbo hilo, Columbia.

Makabiliano kati ya wafungwa yalienea kwa vyumba vitatu vya jela, ambapo watu karibu 1,600 wamefungwa.

Hii ni moja ya mapigano mabaya zaidi katika magereza ya Marekani kwa miaka mingi. Mnamo mwaka 1993, wafungwa watatu na afisa mmoja wa gereza waliuawa katika makabiliano katika jela la Lucasville, katika jimbo la Ohio.