rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Nigeria Mauaji

Imechapishwa • Imehaririwa

Kumi wauawa katika mashambulizi ya makundi yenye silaha Nigeria

media
Jimbo la Zamfara, kaskazini mwa Nigérialinaendelea kukumbwa na machafuko ya makundi yenye silaha. Carte/ RFI

Watu zaidi ya 10 wameuawa katika mashambulizi dhidi ya vijiji, kaskazini mwa Nigeria, eneo linalokabiliwa na machafuko ya makundi ya silaha.


Watu wanaoshukiwa kuwa wezi wa ng'ombe walishambuliwa vijiji vinne siku ya Jumatano katika wilaya Birnin Magaji katika Jimbo la Zamfara, linalokabiliwa na visa vya ulipizaji kisasi kufuatia mauaji ya mmoja wao aliyeuawa na wanamgambo katika jimbo hilo

Kwa mujibu wa msemaji wa polisi wa Jimbo la Zamfara Mohammed Shehu, "watu 10 waliuawa na majambazi", ambao walifyatua risasi hovyo kwa raia.

"Kwa mujibu wa mashahidi, washambuliaji walikimbilia katika msitu wa Rugu katika Jimbo jirani la Katsina," Shehu amesema.

Wakazi wawili wamethibitisha mashambulizi hayo, lakini waliripoti kuwa watu zaidi 26 waliuawa.

"Tulipoteza watu 26 katika mashambulizi dhidi ya (vijiji vya) Dutsin Wake, Oho, Badambaji na Kabingiro," amesema mkazi wa Dutsin Wake Dantani Bube.

Kwa mujibu wa mkazi mwingine akihojiwa kwa njia ya simu, Lawwali Maishanu, watu 17 waliuawa Dutsen Wake, saba Oho, mmoja Badambaji na mwengine mmoja Kabingiro.

Mashambulizi haya yalifuatiwa na mauaji ya "mwizi" aliyeuawa na wanamgambo wa Jimbo hilo katika soko siku chache zilizopita.