Pata taarifa kuu

Wanajeshi 500,000 waliuawa au kujeruhiwa katika vita vya Ukraine

Wanajeshi nusu milioni wanasemekana kuuawa au kujeruhiwa katika vita vya Urusi dhidi ya Ukraine. Ripoti iliyofichuliwa na vyombo vya habari vya Marekani wakati mashambulizi ya Kyiv kuelekea maeneo yanayokaliwa na Moscow yanaonekana kupungua.

Kwa mujibu wa gazeti la New York Times, wanajeshi 500,000 waliuawa au kujeruhiwa wakati wa mapigano kati ya Urusi na Ukraine.
Kwa mujibu wa gazeti la New York Times, wanajeshi 500,000 waliuawa au kujeruhiwa wakati wa mapigano kati ya Urusi na Ukraine. REUTERS - VIACHESLAV RATYNSKYI
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu huko New York, Loubna Anaki

Hasara ni kubwa kwa pande zote mbili. Kwa mujibu wa gazeti la New York Times, ambalo linawanukuu maafisa wakuu wa Marekani, wanajeshi 120,000 wa Urusi na wanajeshi 70,000 wa Ukraine wameuawa tangu Moscow ilipoanzisha mashambulizi yake nchini Ukraine miezi kumi na minane iliyopita.

Takwimu zinaombwa kuthibitishwa

Jumla ya wanajeshi 500,000 kutoka nchi zote mbili waliripotiwa kuuawa au kujeruhiwa katika mapigano hayo. Hata hivyo Gazeti hilo la kila siku linabainisha ni vigumu kuthibitisha takwimu hizi, kwa sababu Urusi ina tabia ya kutokubali au kutotangaza hasara inayopata kwa upande wa jeshi lake, wakati Ukraine inaepuka tu kuchapisha takwimu rasmi. Kwa hivyo makadirio haya yanatokana na picha za satelaiti, udukuzi wa mawasiliano, vyombo vya habari pamoja na ripoti rasmi kutoka kwa serikali hizo mbili.

Hasara kubwa

Kwa mujibu wa maafisa wakuu wa Marekani walionukuliwa na Gazeti la New York Times, Urusi ilipata hasara kubwa zaidi kuliko Ukraine, hasa kwa sababu Moscow ina wanajeshi mara tatu zaidi kwenye uwanja wa vita.

Hasarau kubwa katika vita ambayo tayari imegharimu maisha ya maelfu ya raia na kusababisha mamilioni ya watu kulazimika kuyatoroka makazi yao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.