Pata taarifa kuu

Raia wa Urusi anayeshutumiwa kutoa taarifa za upelelezi kwa Washington ashtakiwa

Robert Chonov, mfanyakazi wa zamani kwenye Ubalozi mdogo wa Marekani huko Vladivostok, anasemekana kuwa alitoa taarifa za mzozo wa kivita kwa Marekani.

Gari likipita karibu na jengo la idara ya Usalama ya Shirikisho la Urusi (FSB) kwenye eneo la Lubyanskaya huko Moscow, Urusi, Jumatatu, Julai 24, 2017.
Gari likipita karibu na jengo la idara ya Usalama ya Shirikisho la Urusi (FSB) kwenye eneo la Lubyanskaya huko Moscow, Urusi, Jumatatu, Julai 24, 2017. AP
Matangazo ya kibiashara

 

Vyombo vya usalama vya Urusi (FSB) vilitangaza Jumatatu Agosti 28 kuwa vimemfungulia mashtaka raia wa Marekani menye asili ya Urusi, mfanyakazi wa zamani wa diplomasia ya Marekani nchini Urusi, aliyekamatwa mwanzoni mwa mwaka na anayetuhumiwa kusambaza taarifa za mzozo wa kivita nchini Ukraine kwa Marekani. 

Wakati ambapo uhusiano kati ya Urusi na Washington, ambayo inaunga mkono Kiev, umedorora, FSB iliomba kuweza kuwahoji wanadiplomasia wawili wa Marekani wanaoshutumiwa katika suala hili, jambo ambalo ni nadra.

Katikati ya mwezi Mei, Moscow ilitangaza kukamatwa kwa Robert Chonov, mfanyakazi wa zamani wa ubalozi mdogo wa Marekani huko Vladivostok (Mashariki ya Mbali), akishutumiwa kwa "ushirikiano wa siri na nchi ya kigeni". Washington ililaani shutuma hizo "zisizo na msingi". Siku ya Jumatatu, katika taarifa kwa vyombo vya habari, FSB ilithibitisha kwamba Robert Chonov alishtakiwa kwa kosa hili, akikabiliwa na kifungo cha miaka minane jela.

Katika taarifa yake, FSB imesema kwamba Robert Chonov alikusanyika tangu Septemba 2022, hadi kukamatwa kwake kwa tarehe isiyojulikana, habari za diplomasia kwa niaba ya Marekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.