Pata taarifa kuu

Marekani imetangaza msaada wa ziada wa dola milioni 400 kwa Ukraine

Nairobi – Wizara ya ulinzi ya Marekani imetangaza msaada wa ziada wa dola milioni 400 kwa Ukraine, ikijumuisha makombora ya ulinzi wa anga, magari ya kivita na ndege ndogo zisizo na rubani, huku mashambulio ya Ukraine dhidi ya Urusi yakiendelea.

Hornets ni ndege ndogo zisizo na rubani ambazo hutumiwa kwa kiasi kikubwa kwa kukusanya habari.
Hornets ni ndege ndogo zisizo na rubani ambazo hutumiwa kwa kiasi kikubwa kwa kukusanya habari. Flir
Matangazo ya kibiashara

Mpango huo mpya wa msaada utajumuisha, kwa mara ya kwanza ndege zisizo na rubani za Black Hornet Nano za Marekani za uchunguzi zilizotengenezwa na Teledyne FLIR Defense.

Hornets ni ndege ndogo zisizo na rubani ambazo hutumiwa kwa kiasi kikubwa kwa kukusanya habari.

Ndege hiyo isiyo na rubani iliyotengenezwa na Norway inatumiwa nchini Ukraine kupitia michango ya serikali ya Uingereza na Norway, kampuni hiyo ilisema.

Silaha zengine ambazo Marekani inaipa Ukraine  ni pamoja na zana za mifumo ya ulinzi wa angani maarufu kama Patriot, pamoja na silaha nyengine inayosema zitaisaidia Ukraine kujilinda kutokana na mashambulio ya Moscow.

Huu ni mpango wa 43 wa msaada wa kiusalama kwa Ukraine kuidhinishwa na Marekani.

Zaidi ya dola bilioni 43 za msaada wa kijeshi wa Marekani zimetolewa tangu uvamizi wa Urusi mwaka 2022.

Haya yanajiri wakati huu idara ya ulinzi ya Ukraine ikidai kupata mafaniko madogo dhidi ya wanajeshi wa Israeli katika eneo la Donetsk. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.