Pata taarifa kuu

Mfahamu Yevgeny Prigozhin, mshirika wa karibu aliyeasi na kuwa adui mkubwa wa Putin

Yevgeny Prigozhin, mkuu wa mamluki wa Urusi Wagner, amejipatia umaarufu kutokana na mchango wake katika vita vya Ukraine, ambapo mamluki wake wanapigana kwa niaba ya Moscow baada ya wanajeshi wa kawaida wa Urusi kukabiliwa na changamoto katika uwanja wa vita ambapo pia walidaiwa kupoteza maeneo hali iliyotajwa kama fedheha kwa utawala wa Moscow.

Kiongozi wa Wagner Yevgeny Prigojine huko Rostov-on-Don, Juni 24, 2023.
Kiongozi wa Wagner Yevgeny Prigojine huko Rostov-on-Don, Juni 24, 2023. via REUTERS - PRESS SERVICE OF "CONCORD\
Matangazo ya kibiashara

Wanajeshi wa Wagner waliweka bendera ya Urusi katika mji wa Bakhmut mashariki mwa Ukraine mwezi Aprili baada ya vita vya muda mrefu na kupata ushindi uliotajwa kuwa mkubwa kwa Urusi katika mzozo huo uliodumu kwa miezi 15.

Siku chache baada ya ushindi huo, mkuu wa Wagner aliwashtumu wakuu wa jeshi la Urusi kwa changamoto walizokabiliwa nazo nchini Ukraine, swala ambalo ni watu wachache wanaweza kulifanya bila kukabiliwa na utawala wa Kremlin.

Picha ya ndege ya Urusi iliyoanguka, ambayo Yevgeny Prigozhin alikuwa ndani, mnamo Agosti 23, 2023.
Picha ya ndege ya Urusi iliyoanguka, ambayo Yevgeny Prigozhin alikuwa ndani, mnamo Agosti 23, 2023. via REUTERS - OSTOROZHNO NOVOSTI

Mzozo kati ya wizara ya ulinzi ya Urusi na wapiganaji wa Wagner ulifikia kiwango kipya siku ya Jumamosi wakati kiongozi wake alipodai wapiganaji wake walivuka kutoka Ukraine na kuingia katika mji wa mpakani wa Urusi wa Rostov-on-Don - na kwamba wangepambana na yeyote atakayejaribu kuwazuia.

Katika hotuba ya dharura ya televisheni, Rais wa Urusi Vladimir Putin alisema kwamba "maasi ya kutumia silaha" ya Wagner yalikuwa sawa na uhaini na kwamba mtu yeyote ambaye amechukua silaha dhidi ya jeshi la Urusi ataadhibiwa.

Hatua hiyo imekuja siku moja baada ya Prigozhin kumshutumu waziri wa Ulinzi Sergei Shoigu kwa kuamuru shambulio la roketi kwenye kambi za wapiganaji  wa Wagner huko Ukraine, na kuua "idadi kubwa" ya wapiganaji wake.

Asili ya Prigozhin

Prigozhin, 62, alipatikana na hatia ya wizi na shambulio mnamo 1981 na akahukumiwa miaka 12 jela. Kufuatia kuachiliwa kwake, alifungua biashara ya mikahawa huko Saint Petersburg katika miaka ya 1990.

Ilikuwa katika nafasi ambapo alipata kujuana na rais Putin, wakati huo akiwa naibu meya wa jiji hilo.

Alitumia nafasi hiyo hiyo kuendeleza biashara ya upishi na akashinda kandarasi za faida za serikali ya Urusi ambazo zilimpa jina la utani, "mpishi wa Putin".

Mnamo Januari, Prigozhin alikubali kuanzisha, kuongoza na kufadhili kampuni ya Wagner ya kivuli.

Alisema alikuwa na wanaume 50,000 "katika nyakati bora," na karibu 35,000 kwenye mstari wa mbele wakati wote.

Hakusema ikiwa nambari hizi zilijumuisha wafungwa, lakini anajulikana kuwa alitembelea magereza ya Urusi kuajiri wapiganaji, na kuahidi msamaha ikiwa wangenusurika katika safari ya nusu mwaka ya jukumu la mstari wa mbele na Wagner.

Sio mgeni katika magereza ya Urusi, aliajiri maelfu ya wahalifu waliohukumiwa kutoka jela kwa ajili ya kundi lake la Wagner - bila kujali uhalifu wao ni mkubwa kiasi gani - mradi tu walikubali kupigana kwa ajili yake nchini Ukraine.

Kabla ya Urusi kuanza mzozo ambao umekuwa mbaya zaidi barani Ulaya tangu Vita vya Pili vya Dunia, Prigozhin alishutumiwa kwa kuingilia uchaguzi wa Marekani na kupanua ushawishi wa Urusi barani Afrika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.