Pata taarifa kuu

Urusi: Mkuu wa Wagner Yevgeny Prigozhin afariki dunia katika ajali ya ndege

Ndege ya kibinafsi iliyokuwa na watu kumi imeanguka Jumatano Agosti 23 katika eneo la Tver, Urusi, ilipokuwa ikisafiri  kati ya Moscow na Saint Petersburg, na kuua watu wote waliokuwa ndani ya ndege hiyo, idara ya huduma za dharura imetangaza. Kulingana na mashirika ya habari ya Urusi Ria Novosti, TASS na Interfax, Mkuu wa kundi la mamluki wa Urusi la Wagner  Yevgeny Prigozhin alikuwa kwenye orodha ya abiria hao.

Yevgeny Prigozhin mnamo Aprili 8, 2023 huko Moscow. Kiongozi wa Kundi la Wagner anakisiwa kufariki katika ajali ya ndege mnamo Agosti 23, 2023.
Yevgeny Prigozhin mnamo Aprili 8, 2023 huko Moscow. Kiongozi wa Kundi la Wagner anakisiwa kufariki katika ajali ya ndege mnamo Agosti 23, 2023. REUTERS - YULIA MOROZOVA
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na shirika la usafiri wa anga la Urusi, jina la Yevgeny Prigozhin lilikuwa kwenye orodha ya abiria ya ndege iliyokuwa ikiruka kutoka Moscow kwenda Saint Petersburg ambayo ilianguka katika eneo la Tver, chini ya kilomita 200 kutoka mji mkuu. Waokoaji wanasema hakuna hata mmoja wa watu waliokuwa ndani ya ndege hiyo aliyenusurika kwenye ajali hiyo.

"Kulikuwa na watu 10 ndani ya ndege, wakiwemo wafanyakazi watatu. Kulingana na habari ya kwanza, watu wote waliokuwemo kwenye ndege hiyo wamefariki, "Wizara ya Hali ya Dharura ya Urusi imesema kwenye Telegram. Ndege hiyo ilianguka karibu na kijiji cha Kujenkino, kaskazini magharibi mwa Moscow.

Mkuu wa kundi la wanamgambo wa Urusi la Wagner, ambalo limekuwa likifanya kazi katika baadhi ya nchi za Kiafrika na katika vita vinavyoendelea tangu Februari 2022 huko Ukraine, Yevgeny Prigozhin hivi karibuni alisimama dhidi ya makao makuu ya jeshi la Urusi Urusi na Waziri wa Ulinzi, Sergei Shoigu. Mnamo mwezi Juni, aliongoza uasi na wapiganaji wake na kuelekea Moscow. Aliachana na uasi huu baada ya saa chache, tarehe 24 Juni.

Jumatatu Agosti 21, Yevgeny Prigozhin alionekana kwenye video na iliyorushwa na makundi yaliyo karibu na kundi la Wagner. Video hiyo ilionyesha Prigozhin katikasare za kijeshi , akisema kundi hilo linaifanya Afrika "huru zaidi".

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.