Pata taarifa kuu

Urusi yakubali kurudi kwenye makubaliano ya nafaka kama marsharti yake yatazingatiwa

Urusi kupitia Yury Ushakov, msaidizi wa Rais Putin, imesema kuwa haijajiondoa moja kwa moja kwenye mkataba wa nafaka, huku ikibani kwamba iko tayari kurudi kwenye mkataba huo ikiwa masharti yake yatazingatiwa, ikiongeza kuwa mkataba huo haujakatizwa kabisa.

Foleni ya malori ya zaidi ya kilomita kumi katika kituo cha ukaguzi huko Rava-Ruska kwenye mpaka wa Ukraine na Poland, Aprili 18, 2023.
Foleni ya malori ya zaidi ya kilomita kumi katika kituo cha ukaguzi huko Rava-Ruska kwenye mpaka wa Ukraine na Poland, Aprili 18, 2023. AFP - YURIY DYACHYSHYN
Matangazo ya kibiashara

Yury Ushakov amebaini kwamba mpango wa mkataba huo haujapunguzwa kabisa, umesitishwa tu.

"Tuko tayari kurudi ushiriki majukumu ambayo yalikubaliwa upande wa Urusi yatatekelezwa kwa vitendo", amesema Yury Ushakov, msaidizi wa Rais Putin.

Mkataba uliokuwa unatoa nafasi kwa usafirishwaji salama katika Bahari Nyeusi wa nafaka za Ukraine kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita, ulifikia mwisho siku ya Jumatatu Julai 17, 2023.

Mkataba huo ulifikia kikomo baada ya Urusi kujiondoa na kutahadharisha kwamba haiwezi kuhakikisha usalama wa meli zitakazokuwa zinasafirisha nafaka katika bahari hiyo nyeusi.

Mkataba huo wa usafirishaji wa nafaka ulifikiwa mwaka jana chini ya usimamizi wa Uturuki na Umoja wa Mataifa kusaidia kukabiliana na mzozo wa chakula uliokuwa unaikumba dunia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.