Pata taarifa kuu

Urusi: Magavana wataweza kuunda wanamgambo wa kibinafsi katika baadhi ya hali

Bunge la Urusi (Duma) limepiga kura siku ya Jumanne alasiri Julai 25 kwenye moja ya hatua za kwanza za marekebisho ya ukomo wa umri wa kujiandikisha. Zoezi la kujiandikisha litaanza Januari 1, 2024, kuanzia miaka 27 hadi 30. Umri wa chini unapaswa pia kuinuliwa, baadaye, kutoka miaka 18 hadi 21. Lakini kinachovutia macho ni marekebisho yaliyoongezwa muda katka dakika za mwisho: uwezekano wa magavana kuunda kampuni za kijeshi za kibinafsi.

Makao makuu ya Bunge la Urusi (Duma), sehemu iliyopigwa  picha katikati mwa Moscow Jumanne hii Julai 25, 2023.
Makao makuu ya Bunge la Urusi (Duma), sehemu iliyopigwa picha katikati mwa Moscow Jumanne hii Julai 25, 2023. AFP - ALEXANDER NEMENOV
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu huko Moscow,

Kwenye karatasi, inaweza kusikika kama "Wagner wa mkoa". Lakini tangu kushindwa kwa uasi mwezi Juni, bila shaka ni suala la kuanza tena kudhbiti na kuunda kundi la wanamgambo watakaoshirikiana na vikosi vya uinzi na usalama katika vita vya Ukraine. Kwa kweli, makampuni haya ya kijeshi yatakuwa chini ya usimamizi wa serikali, na kusimamiwa zaidi.

Kazi yao? “Visaidie vyombo vya usalama katika ulinzi wa utulivu wa umma, mapambano dhidi ya wahujumu na makundi haramu yenye silaha. "

Bila shaka, wanachama wao watakuwa na haki ya kubeba silaha. Lakini hapa tena, matumizi yao yatadhibitiwa madhubuti: kudungua tu ndege zisizo kuwa na rubani, kujibu shambulio la silaha au dhidi ya maeneo yaliyolindwa.

Nani atatoa silaha hizi? Sheria inataja "chombo kilichoidhinishwa na serikali ya shirikisho" kisicho wazi. Watumiaji wa silaha hizo, kwa vyovyote vile, watalazimika kuzirejesha katika tukio la kufutwa kwa shirika lao kwa amri ya rais, ndani ya siku thelathini.

Kila kitu lazima pia kitoke kwa ofisi ya rais: kisheria, makampuni haya yatakuwa makampuni ya serikali. Vladimir Putin pekee ndiye ataweza kuidhinisha orodha ya mikoa iliyoidhinishwa kuwa makampuni haya. Na hii, katika mazingira matatu tu maalum: sheria ya kijeshi, hali ya vita, uhamasishaji.

Uhamasishaji umesimamishwa rasmi kwenye karatasi leo nchini Urusi. Lakini amri iliyoizindua, iliyotiwa saini karibu mwaka mmoja uliopita, bado inatumika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.