Pata taarifa kuu

Ukraine: Watatu wafariki na wengine 10 kujeruhiwa katika shambulio la boti

Watu watatu wameuawa na wengine 10 kujeruhiwa siku ya Jumapili katika shambulio dhidi ya meli moja iiyokuwa njiani ikibeba watu waliokuwa wakihamishwa kutokana na mafuriko kusini mwa Ukraine, gavana wa jimbo hilo amesema.

Херсон после разрушения Каховской ГЭС, Украина. 10 июня 2023.
Херсон после разрушения Каховской ГЭС, Украина. 10 июня 2023. REUTERS - STRINGER
Matangazo ya kibiashara

"Watu kumi na watatu ni waathiriwa wa shambulio la boti lililokuwa likiwahamisha watu kutoka ukingo wa kushoto (wa Mto Dnieper). Raia watatu wameuawa, wengine 10 wamejeruhiwa, wakiwemo maafisa wawili wa vikosi vya usalama,” gavana wa eneo la Kherson Oleksandr Prokudin amesema kwenye Telegram.

Hayo yanajiri wakati wanajeshi wa Ukraine wanaripotiwa kusonga mbele mashariki karibu na Bakhmut na kusini karibu na Zaporizhzhia, na wamefanya mashambulizi ya masafa marefu kulenga maeneo ya Urusi.

Lakini kutathmini hali halisi vitani ni vigumu, huku pande mbili zinazozozana zikiwasilisha simulizi zinazotofautiana: Ukraine ikidai kusonga mbele na Urusi ikisema inapambana na kufanya mashambulizi.

Wakati huo huo katika eneo la Kaluga nchini Urusi - ambalo linapakana na wilaya za kusini karibu na Moscow - gavana Vladislav Shapsha alisema kwenye mtandao wa Telegram kwamba ndege isiyo na rubani ilianguka karibu na kijiji cha Strelkovk mapema siku ya Jumapili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.