Tetemeko la Ardhi: Uturuki yasitisha utafiti isipokuwa katika majimbo mawili
Uturuki imeamua siku ya Jumapili, siku kumi na nne baada ya tetemeko la ardhi la Februari 6, kusitisha zoezi la kutafuta miili isipokuwa katika majimbo mawili yaliyoathiriwa zaidi, Kahramanmaras na Hatay, imetangaza shirika la misaada la serikali (Afad).
Imechapishwa:
Matangazo ya kibiashara
“Katika mikoa mingi juhudi za kutafuta miili limemalizika. Wanaendelea katika majimbo ya Kahramanmaras na Hatay, karibu na majengo arobaini”, ametangaza Unus Sezer, mkuu wa Afad.
Tetemeko la ardhi la kipimo cha 7.8 lililoharibu kusini mwa nchi hiyo na Syria liliua watu 40,689 nchini Uturuki, kulingana na ripoti rasmi ya hivi punde iliyotolewa na Afad siku ya Jumapili.