Chama cha Kurdistan's Workers' Party (PKK) chahusihwa na shambulio baya Istanbul
Waziri wa Mambo ya ndani wa Uturuki, Suleyman Soylu amekishtumu chama cha Kurdistan's Workers' Party (PKK) kwa kuhusika na shambulio la bomu jijini Istanbul na kusababisha vifo vya watu sita na kuwajeruhi wengine zaidi ya 80.
Imechapishwa:
Pamoja na shutuma hizi, Waziri huyo amesema mmoja wa watu waliohusika na shambulio anayeaminiwa kutega bomu himo, amekamatwa.
Shambulio hilo lilitokea katika barabara yenye shughuli nyingi ya Istiklal hapo jana.
Uturuki, imeiorodhesha chama cha PKK kama shirika la kigaidi linaloungwa mkono na mataifa ya nje.
Rais Recep Tayyip Erdogan naye pia amelaani shambulio hilo alilosema dalili zote zimeonesha kuwa ni kla kigaidi.
Mwaka 2015, shambulio lingine lilitokea katika barabara hiyo ya Istiklal wakati wa kampeni za kisiasa, na nchi hiyo imekuwa ikishuhudia matukio lama haya ambayo yamehusishwa na kundi la Islamic State.