Recep Tayyip Erdogan: Ninaami kwamba Putin ana nia ya kumaliza vita nchini Ukraine
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, amesema anaamini kuwa rais wa Urusi Vladimir Putin, anatafuta mbinu ya kumaliza vita alivyoanzisha nchini Ukraine, na hatua kubwa itachukuliwa.
Imechapishwa:
Rais Erdogan amesema, kwa kuzingatia mazungumzo aliyokuwa nayo na kiongozi huyo wa Urusi, anapenda vita hivyo vimalizike haraka iwezekanavyo.
Aidha, Erdogan amesema baada ya mazungumzo yake na Putin wiki iliyopita, vita vinavyoendelea nchini Ukraine vinaonekana kumsumbua.
Kauli hii ya kiongozi huyo wa Uturuki, imekuja wakati huu Ukraine ikiendelea kuchukua baadhi ya maeneo Mashariki mwa nchi yake, iliyokuwa inashikiliwa na wanajeshi wa Urusi.
Wakati hayo yakijiri, Kyiev imeapa kuondoa vitisho kutoka Moscow baada ya majimbo mawili yanayodhibitiwa na wanajeshi wa Urusi, kutangaza mpango wa kuwa na kura za maoni, kuwa sehemu ya Urusi wiki hii.