Pata taarifa kuu

Msaada wa China kwa Urusi: Beijing yashutumu habari potofu za Marekani

China imeshutumu habari potofu kutoka kwa Marekani baada ya vyombo vya habari vya Marekani kuripoti kwamba Moscow iliomba msaada wa kijeshi na kiuchumi wa China ili kukabiliana na vikwazo vya Magharibi dhidi ya vita vyake nchini Ukraine.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa China Zhao Lijian.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa China Zhao Lijian. AP - Liu Zheng
Matangazo ya kibiashara

"Hivi karibuni, Marekani imekuwa ikieneza habari za uongo dhidi ya China," msemaji wa Wizara ya Mmbo ya Nje wa China Zhao Lijian amewaambia waandishi wa habari alipoulizwa kuhusu habari kutoka Gazeti la "New York Times".

Mshauri wa Usalama wa Kitaifa wa Marekani Jake Sullivan aliionya Beijing siku ya Jmapili kupitia vyombo vya habari kwamba China haiwezi kuisaidia Urusi kukwepa vikwazo vya kiuchumi bila kupata madhara yoyote. Ili kuhalalisha tuhuma zake, utawala wa Biden uliambia gazeti kuu la kila siku la Marekani jana kwamba Urusi iliiomba China msaada na vifaa vya kijeshi hasa.Awali Ikulu ya Marekani -White House ilionya kuwa Beijing itakabiliwa na matokeo makali ikiwa itaisaidia Moscow kuvikwepa vikwazo.

Gazeti New York Times limeandika msaada ya Urusi una lengo la kukabiliana na makali ya vikwazo vilivyowekwa na mataifa ya Magharibi. Hata hivyo maafisa hao wamekataa kutoa ufafanuzi wa mambo gani hasa ambayo Urusi imeyaomba au kama China imeyatolea majibu maombi hayo. Ubalozi wa China mjini Washington umekanusha madai hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.