Cyprus: UNSC yalaani mpango wa kufungua tena Varosha
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeshtumu katika taarifa Ijumaa hatua ya Uturuki na Cyprus ya Uturuki kufunuliwa kwa upande mmoja wa sehemu ya Varosha na kutaka kufutwa kwa hatua hii mara moja.
Imechapishwa:
"Baraza la Usalama linasisitiza umuhimu wa kuzuia hatua yoyote ya upande mmoja ambayo inakwenda kinyume na maazimio yake na ambayo inaweza kuongeza mvutano katika kisiwa (cha Cyprus) na kudhoofisha matarajio ya suluhu," wajumbe Kumi na Tano wa baraza hilo wamesema.
Katika ziara yake siku ya Jumanne katika mji mkuu uliogawanyika wa kisiwa cha Mediterranean, kuadhimisha udhibiti wa sehemu ya kaskazini ya Cyprus na jeshi la Uturuki Julai 20, 1974, rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan alitangaza kuendelea na zoezi la kufunguliwa kwa mji wa Varosha (Maras kwa Kituruki), eneo la kale la mapumziko ambalo kutelekezwa kwake kunaashiria mgawanyiko wa kisiwa hicho.
Cyprus imegawanyika tangu mwaka1974 kati ya sehemu ya Uigiriki inayotambuliwa na Umoja wa Ulaya na sehemu ya Uturuki isiyotambuliwa na jamii ya kimataifa, isipokuwa Ankara.