Pata taarifa kuu
CYPRUS

Marekani yafutilia mbali suluhisho la serikali mbili kwa Cyprus

Marekani imepinga suluhisho la serikali mbili kwa Cyprus iliyoshinikizwa siku za hivi karibuni na rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, afisa mwandamizi katika wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, Victoria Nuland, amesema leo Jumatano.

Rais wa Uturuki Erdogan mbele ya Wabunge wa Jamhuri ya Uturuki ya Cyprus ya Kaskazini, kaskazini mwa Nicosia, Cyprus, Julai 19, 2021.
Rais wa Uturuki Erdogan mbele ya Wabunge wa Jamhuri ya Uturuki ya Cyprus ya Kaskazini, kaskazini mwa Nicosia, Cyprus, Julai 19, 2021. via REUTERS - Murat Cetinmuhurdar/PPO
Matangazo ya kibiashara

Alipoulizwa wakati wa kikao cha bunge, ikiwa serikali ya Marekani imefutilia mbali chaguo kama hilo, amejibu: "ndio, kabisa". "Tunachoamini ni kuwa mchakato unaoongozwa na Wacyprus, wa pande mbili na wa kawaida, ndio ambao unaweza kuleta amani na utulivu huko Cyprus", amesema.

Mvutano wa kisiwa cha Cyprus kilichogawika umechukua mwelekeo mpya baada ya Cyprus ya upande wa Uturuki kuchukua sehemu ya mji wa Varosha uliotelekezwa miaka 47 iliyopita kwa lengo la kuanzisha makaazi ya raia wake.

Cyprus yawasilisha suala la mvutano wa kisiwa mbele ya baraza la usalama la UN

Kwa mujibu wa waziri wa mambo ya nje wa Serikali ya Cyprus iliyoko mjini Nicosia inayotambulika kimataifa imelipeleka suala la mvutano wa kisiwa hicho mbele ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, kuhusiana na suala la kuchukuliwa kwa sehemu ya mji wa pwani uliotelekezwa miaka 47 iliyopita wa Varosha na Cyprus ya Uturuki.

Maafisa wa Cyprus ya Uturuki na Uturuki yenyewe, Jumanne wiki hii, walitangaza kwamba sehemu ndogo ya mji huo wa Varosha  itakuwa chini ya mamlaka ya raia kwa ajili ya uwezekano wa kuanzisha makaazi mapya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.