Pata taarifa kuu
ITALIA-CORONA-AFYA

Italia kuanza kulegeza vizuizi vya kupambana na Corona Mei 4

Waziri Mkuu wa Italia Giuseppe Conte ametangaza kuwa nchi hiyo itaanza kurejea polepole katika hali yake ya kawaida kuanzia tarehe 4 mwezi Mei, wakati huu nchi hiyo ikiendelea kupambana na maambukizi ya Corona.

Waziri Mkuu Conte amewataka wananchi wa taifa hilo watakapoanza kutoka nje, wavae barakoa na kuepuka kupeana mikono na kukumbatiana.
Waziri Mkuu Conte amewataka wananchi wa taifa hilo watakapoanza kutoka nje, wavae barakoa na kuepuka kupeana mikono na kukumbatiana. Tiziana FABI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Conte ameaahidi raia wa nchi yake kuwa hivi karibuni watapata nafasi ya kutoka makwao na kuenda kutembea katika maeneo ya umma na hata kwenda kuwatembelea ndugu zao.

Aidha, amesema kuwa shule zitaanza kufunguliwa kufikia mwezi Septemba lakini shughuli za kibiashara zitarejelewa tena baada ya wiki tatu zijazo.

Mitaa ya Italia ikisalmia tupu kutokana na vizuizi vya maambukizi ya virusi vya Corona vilivyowekwa na serikali.
Mitaa ya Italia ikisalmia tupu kutokana na vizuizi vya maambukizi ya virusi vya Corona vilivyowekwa na serikali. REUTERS/Antonio Parrinello

Pamoja na hakikisho hili, Waziri Mkuu Conte amewataka wananchi wa taifa hilo watakapoanza kutoka nje, wavae barakoa na kuepuka kupeana mikono na kukumbatiana.

Hata hivyo uamuzi wa lini ligi kuu ya soka nchini humo Serie A, itaanza tena, hilo halijaafikiwa.

Tangu kuzuka kwa maambukizi ya Corona nchini Italia, zaidi ya watu 26,000 wamepoteza maisha na kuwa taifa la pili baada ya Marekani kuwa na idadi kubwa ya watu waliopoteza maisha duniani, lakini ya kwanza barani Ulaya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.