Pata taarifa kuu
ITALIA-CORONA-AFYA

Coronavirus: Italia yarefusha hali ya dharura katika ngazi ya taifa

Serikali ya Italia imetangaza hali ya hatari katika maeneo yote ya nchi hiyo yenye watu zaidi ya Milioni 60 ikiwa ni katika harakati za kuendelea kupambana na ongezeko la maambukizi ya Corona.

Waziri Mkuu wa Italia Giuseppe Conte, Machi 4, 2020 huko Roma.
Waziri Mkuu wa Italia Giuseppe Conte, Machi 4, 2020 huko Roma. TIZIANA FABI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Hatua zilizochukuliwa ni pamoja na kuzuia raia wa nchi hiyo kutembea na kukutana katika maeneo ya umma.

Waziri Mkuu Giuseppe Conte amewataka raia wa nchi hiyo kusalia nyumbani na kuomba kibali maalum iwapo wanataka kusafiri nje ya maeneo yao, hatua ambayo amesema inachukuliwa kwa sababu hakuna muda wa kupoteza kuhusu mapambano dhidi ya virusi hivyo.

Idadi ya watu waliopoteza maisha kutokana na maambukizi haya imeongezeka kutoka 366 hadi 463 na kulifanya taifa la pili lililoathiriwa zaidi na maambukizi haya duniani baada ya China.

Maafisa nchini humo wanasema kuwa majimbo 20 yameathiriwa na maambukizi haya.

Shirika la fya Duniani WHO linasema kuwa watu zaidi ya 3,800 wamepoteza maisha na wengine 110,000 kuambukizwa kote duniani, idadi kubwa wakiwa raia wa China.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.