Pata taarifa kuu
UJERUMANI-EU-MERKEL-USHIRIKIANO

Angela Merkel aonya EU kujidhatiti vilivyo

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema mataifa ya Umoja wa Ulaya sasa ni lazima yachukue jukumu la kuendeleza maendeleo yake wenyewe bila kuangalia nje ya bara hilo.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel autaka Umoja wa Ulaya kupigania mustakabili wake kwanza.
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel autaka Umoja wa Ulaya kupigania mustakabili wake kwanza. REUTERS/Fabrizio Bensch
Matangazo ya kibiashara

Kansela Merkel aliyasema hayo mwishoni mwa wiki iliyopita akiwahotubua raia wa Ujerumani Kusini mwa nchi hiyo baada ya kurejea nyumbani kutoka katika mkutano wa G7 nchini Italia, mkutano ambao haukuwa rahisi kwa wakuu wa nchi hizo saba kubwa kiuchumi duniani.

Ameongeza kuwa hata wakati Umoja wa Ulaya, unapojitahidi kuimarisha uhusiano mzuri na Uingereza na Marekani, lakini ni Umoja huo lazima upiganie mustakabili wake kwanza.

Kauli ya rais wa Marekani Donald Trump ambaye alinukuliwa akilalamika kuwa Ujerumani inauza magari mengi sana nchini Marekani na kusema ni biashara mbaya, hayakumfurahsiha Kansela Merkel.

Wakati huo huo, Merkel na viongozi wenzake watano walikuwa na wakati mgumu kumridhisha rais Trump kuunga utekelezwaji kikamilifu kwa mkataba wa mabadiliko ya hali ya hewa uliokubaliwa jijini Paris mwaka 2015.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.