Joto la kisiasa linazidi kupanda nchini Marekani kuelekea uchaguzi wa mwezi Novemba 2016 baada ya vyama vikuu vya siasa Republican na Democrat kupata wagombea wake Hillary Clinton na Donald Trump na kila mmoja akijinadi katika kampeni ili kuwashawishi Wamarekani wamuunge mkono. Je ni Hillary Clinton au Donald Trump atakayemudu kuvaa viatu vya Rais Barack Obama? Kupata mengi zaidi na katika Makala ya Wimbi la Siasa na Victor Robert Wile.
Vipindi vingine
-
Wimbi la siasa: Madai ya Burundi kwa Rwanda kuhusika na vitendo vya uhalifu nchini Burundi
Kwenye Makala haya Ali Bilali akiwa pamoja na wachambuzi wa siasa Mali Ali kutoka Paris Ufaransa na Abdulkarim Atiki wanaangazi kuhusu tuhuma za Burundi kwa Rwanda kuhusika na vitendo vya uhalifu hususan uvurumishaji guruneti katika mji wa Bujumbura, tukio la hivi karibuni liligharimu maisha ya watu kadhaa na kuwajeruhi wengine.17/05/202410:01 -
Serikali ya Sudan Kusini na makundi ya waasi yaanza mazungumzo jijini Nairobi
Mazungumzo ya amani yanayohusisha makundi ya waasi nchini Sudan Kusini na serikali yameanza rasmi jijini Nairobi, wakati huu taifa hilo likijiandaa kwa uchaguzi wa mwezi Disemba.10/05/202410:05 -
Nini haki za wafanyakazi duniani ?
Kila tarehe 1, ni maadhimisho ya sikukuu ya wafanyakazi duniani. Wafanyakazi wanatumia siku hii kusherehekea mafanikio yao na kuendeleza mapambano ya haki zao. Je, siku hii ina umuhimu gani ? Wageni wetu ni Nice Mwansasu kutokaΒ Β Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) na mwanasheria wa masuala ya ajira kutoka Kenya Elvis Abenga01/05/202410:13 -
Mwaka mmoja wa mapigano nchini Sudan kati ya jeshi la serikali na RSF
Wiki hii, ilikuwa ni mwaka mmoja wa vita nchini Sudan, kati ya jeshi la taifa chini ya JeneraliΒ Abdel Fattah al-Burhan na wanamgambo wa RSF wanaongozwa na Jenerali Mohammed Hamdan Dagalo.17/04/202409:34 -
Maadhimisho ya miaka 30 ya mauaji ya kimbari nchini Rwanda ,ulimwengu umejifunza nini?
Kumbikizi ya miaka 30 tangu mauaji ya kimbari yaliyosababisha vifo vya watu hadi laki 8 ,kuna wito wa ulimwengu kuhakikisha watuhumiwa zaidi kusakwaΒ na mataifa yaweke mikakati kuzuia mauaji kama haya kutojirudia03/04/202409:48