Pata taarifa kuu
Wimbi la Siasa

Nini kinafuata nchini Syria kufuatia kuchaguliwa tena kwa rais Bashar al-Assad

Imechapishwa:

Wimbi la siasa juma hili linaangazia uchaguzi mkuu wa urais nchini Syria ambapo kwa awamu nyingine wananchi wa taifa hilo wamerudisha madarakani rais Bashar al-Assad kuongoza taifa hilo kwa kipindi cha miaka 7 ijayo.

Rais Bashar al-Assad akipiga kura hivi karibuni kwenye kituo cha mjini Damascus
Rais Bashar al-Assad akipiga kura hivi karibuni kwenye kituo cha mjini Damascus REUTERS/SANA/Handout via Reuters
Matangazo ya kibiashara

Waasi wa Syria wakiondoka kwenye mji wa Homs
Waasi wa Syria wakiondoka kwenye mji wa Homs REUTERS/Ghassan Najjar

Uchaguzi wa mwaka huu nchini Syria ulisusiwa na Baraza la Kitaifa la Upinzani nchini humo kwa kile viongozi wake wanachodai kuwa uchaguzi huo haukuwa huru na haki kwakuwa rais Assad bado ameendelea kung'ang'ania madarakani.

Sio upinzani pekee ambao ulisusia uchaguzi wa mwaka huu lakini hata mataifa ya Ulaya na Marekani isipokuwa China na Urusi yalisusia uchaguzi mkuu uliofanyika nchini Syria.

Upinzani ulitaka uchaguzi huo usifanyike kwanza mpaka pale suluhu ya kisiasa ingepatokana nchini humo kwakuwa bado walikuwa kwenye mazungumzo na utawala wa Assad chini ya Usimamizi wa Umoja wa Mataifa.

REUTERS/Omar Sobhani

Mzozo huu umekuwa mgumu kuusuluhisha kwakuwa hata mataifa ya magharibi yenyewe yamegawanyika kuhusu mzozo wenyewe na namna bora ya kuutatua hali iliyopelekea hata msuluhishi wa Umoja wa Mataifa, Lakhdar Brahimi nae kutangaza kujiondoa.

Mtangazaji wa makala hii juma hili ameangazia mustakabali wa taifa hili kisiasa hasa mara baada ya rais Assad kuchaguliwa tena kuliongoza taifa hilo kwa muhula mwingine wa miaka 7.

Vipindi vingine
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.